UĎSM WACHAKATA MAGANDA YA MATUNDA KUTENGENEZA BIDHAA ZA NISHATI NA MAABARA

Dk.JOVIN EMMANUEL AKIONYESHA MOJA YA BIDHAA ZILIZOCHAKATWA KUTOKANA NA MATUNDA


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha Dar esalaam(UDSM) wamefanya utafiti wa maganda ya matunda ikiwemo papai nanasi,embe na tikiti maji na kupata bidhaa tofauti ambazo zinaweza kutumika kama mafuta ya taa, vitakasa mikono,nishati mbadala ya mafuta ya kwenye magari,spiriti na matumizi ya kwenye maabara.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara  Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Jovin Emmanuel amesema bidhaa hizo zinaenda sambamba na utunzaji wa mazingira kwani kinachotumika ni takataka ambazo huwa zinatupwa.

Amesema watu wengi wamekuwa wakiona takataka hazina faida Kwa hiyo tunazichukua na kutengeneza bidhaa ambazo ni muhimu kwa matumizi ya binadamu ambazo zinakuwa katika viwango tofauti.


Amesema bidhaa hiyo ipo tayari kwa matumizi kwa sababu imeshafanyiwa utafiti isipokuwa changamoto iliyopo ni mtaji wa kitengeneza bidhaa hiyo kwa wingi.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kuwasihi wadau na taasisi mbalimbali kikiwemo chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kufadhili mradi huo ili bidhaa hizo ziweze kuzalishwa kwa wingi na tafiti hiyo ilete matokeo chanya yaliyokusudiwa kwa bidhaa kufika hadi kwa wananchi kwa ajili ya matumizi.

Aidha amesema kwa sasa kama kuna mtu anahitaji moja ya bidhaa hizo kwa matumizi ya ofisini na majumbani anatengezewa kwa oda maalum.

Dkt.Emmanuel amesema wanayatumia maonesho hayo kutangaza bidhaa hizo huku akiwaasa wadau mbalimbali kupita kwenye banda lao kujionea bidhaa hizo.

Chapisha Maoni

0 Maoni