Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
CHUO Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeibuka kidedea kwa kupokea tuzo ya mshindi wa kwanza kwa upande wa taasisi za elimu ya juu nchini katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Kupitia tunzo hiyo UDOM imeishukuru Tantrade kwa kuona juhudi zao kubwa zinazofanywa na chuo hicho na kustahili kupata tuzo hiyo ambayo kwao itawapa chachu ya kuongeza juhudi katika kukiboresha chuo zaidi.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Shahada za Awali UDOM,Dk. Victor Marialle, amesema tuzo hiyo ni ishara ya kutambulika kwa kazi nzuri wanazozifanya zikiwemo bunifu za teknolojia na baadhi ya bidhaa zilizotokana na tafiti kwa ushirikiano walimu na wanafunzi
Amesema UDOM kwa kufanya tafiti mbalimbali zitaifikisha nchi mbali kwani wamedhamiria kufanya tafiti zaidi na kuzigeuza kuwa bidhaa zitakazoingia sokoni kwa lengo la kutatua changamoto zilizoko kwenye jamii.
Marialle amesema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na walimu wamekuwa wakifanyia tafiti hizo kwa vitendo na si darasani pekee na kupata matokeo chanya.
Katika banda hilo katika maonesho ya 48 UDOM waliweza kuleta tafiti mbalimbali ikiwemo mchakato wa kurusha satellite itakayosaidia katika masuala ya mawasiliano, vyombo vinavyoweza kusaidia kupunguza ajali, bunifu zinazoweza kusaidia ulishaji wa samaki na kutoa huduma za lishe.
Pia katika banda hilo zilionekana sanaa bunifu ya picha ya Rais Samia Suluihu Hassan iliyokuwa kivutio kikubwa ilikuwa ikionekana katika mionekano mitatu katika picha moja.
Aidha Marialle aliwataka wanafunzi wa ndani ya nje ya nchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na chuo hicho ili waweze kutoka na elimu ambayo iataweza kuwaidia katika maisha yao.


0 Maoni