Na Pilly Kigome-Nifáhamishe News Blog
CHUO Cha Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinaendelea kuwa kinara kwa kukuza taaluma ya Sanaa na kuongeza ajira kwa wanafunzi wahitimu wa chuo hicho.
Wanafunzi wa fani hiyo katika Chuo hicho wamekuwa wakifundishwa kutumia fursa mbalimbali kupitia rasilimali zinazowazunguka katika mazingira yao katika kujipatia kipato kupitia sanaa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Sanaa na Taaluma za Habari UDOM Dk. Deograsia Ndunguru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba jijini Dar Es Salaam.
Dk Ndunguru amesema wanayatumia maonesho hayo kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo pamoja na wanafunzi katika bunifu mbalimbali ikiwemo picha na chupa zizobadilika kuwa urembo.
Amesema moja ya picha ni ile inayomuonesha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwenye pande tatu ikimzungumzia majukumu yake makubwa hapa nchini.
Amesema kadri unayozunguka kuangalia picha hiyondipoinabadilika na kumuonyesha Rais akiwa katikamavazi matatu tofauti ikiwemo kiremba chekundu inashiria ni Rais, vazi la Kijani na nyeusi ikiashiria kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, na lile vazi la kombati ikiashiria ni Amiri Jeshi Mkuu.
Dk.Ndunguru amesema picha hiyo ambayo imekuwa kivutio kikubwa katika banda hilo imechorwa na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Taaluma ya sanaa Enock Tarimo.
Aidha Ndunguru ametoa wito kuwaasa wanafunzi kujiunga na fani hiyo katika ngazi za elimu ya juu, kusoma hata kozi fupi ili waweze kupata ujuzi wa kutosha na kujitengeneza ajira.
Mhitimu wa UDOM 2023 Sultan Samwel ambaye amejiajiri katika kampuni yake ya mambo ya sanaa Talnis Creative Agency, ametembelea banda hilo na kufurahishwa kuona picha zake alizochora akiwa shuleni.
"Nimefurahi kukuta picha nilizochora katika moja ya mitihani yangu nikiwa chuoni pamoja picha za wanafunzi wenzangu, kimsingi niseme tu sanaa ni ajira kama zilivyofani nyingine kama daktari au sheria na nyingine nyingi,kama hivi mimi nimejiajiri katika kampuni yangu


0 Maoni