TAMASHA LA 27 ZIFF KUANZA AGOSTI 1 FILAMU 60 ZACHAGULIWA


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

TAMASHA la 27 la Kimataifa la filamu Zanzibar ZIFF limepitisha filamu 60 kati ya 3000 zilizopokelewa kutoka sehemu mbalimbali duniani zitakazoshindanishwa katika maonesho hayo.

Filamu zilizochaguliwa ni pamoja na filamu za urefu 17, hali halisi 13, filamu fupi na katuni 30 ambazo zimeteuliwa na wataalamu wabobezi kwa kamati ya uteuzi waliotumia vigezo vinavyoakisi kauli mbiu ya mwaka huu kuhuishwa.

Hayo yamesemwa na CEO wa ZIFF, Joseph Mwale Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bango la tamasha lenye mtazamo wa kisanii la tamasha hilo.

Amesema tamasha hilo la kimataifa Zanzibar lina hadhi kubwa kwenye tasnia ya filamu limekuza mabadiliko ya tamaduni na kusherehekea maboresho ya sanaa ya kutengeneza filamu.

Amefafanua tamasha hilo lilianza mwaka 1997 limekuja kuwa jukwaa kubwa la kuwaunganisha wadau wa filamu duniani kupitia filamu.

Mwale amesema mwaka huu tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 1 hadi 4 lina lengo la kuongeza uelewa wa tasnia ya filamu na kukuza sanaa Barani Afrika na kwa nchi za majahazi za Bahari Hindi ambapo mwakahuu ZIFF itakuwa na program ya siku ya kitaifa ya Zanzibar Julai 31 kutaonyeshwa filamu za kuvutia za Zanzibar pamoja na nyumba ya ajabu.

Pia mwakahuu ZIFF inashirikiana na mkutano wa kimataifa wa vijana wa vyombo vya habari (IYMS) lenye kengo la kuhamasisha vijana ulimwenguni kutumia filamu na vyombo vya habari taarifa kuhamasisha kuelimisha na kuendesha hatua juu ya masuala muhimu ya kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa Tamasha ZIFF Hatibu Maduda amesema tamasha hilo lina lengo kuongeza uelewa watasnia ya filamu na kukuza sanaa barani Afrika na kwa nchi za majahazi na Bahari ya Hindi ikiwemo Asia ya Kusini Mashariki, Rasi ya Uarabuni, Ghuba ya Uajemi,Iran, Pakistan, India na Visiwa vya Bahari ya Hindi.

Aidha amesema kwa mara ya kwanza katika tamasha hilo kutakuwa na majukwaa mbalimbali ikiwemo Jukwaa la watoto, wanawake wa vijijini, mbio za ngalawa, mpira wa miguu wa wanawake ufukweni, majadiliano magumu, jukwaa la muziki na sanaa pamoja na majukwaa ya wazi ya uonyeshaji wa filamu.

Amesema tamasha linatarajiwa kuwa na watazamaji zaidi ya laki mbili (200,000) na kuongeza uelewa wa tasnia ya filamu.

Amefafanua mwakahuu aina ya mashindano ya filamu ni ile filamu bora ya urefu, filamu bora ya hali halisi, tuzo ya Emerson kwa filamu bora Zanzibar, filamu fupi bora, filamu bora ya Afrika Mashariki, mwigizaji bora Afrika Mashariki, mwigizaji bora wa kike Afrika Mashariki, mwigizaji bora Tanzania, mwigizaji bora wa kike Tanzania, tuzo ya mwenyekiti wa ZIFF na tuzo ya mafanikio ya masiha pamoja na tuzo ya chaguo la watu ambayo inahifadhiwa kwa mfululizo wa drama za televisheni kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC).

Chapisha Maoni

0 Maoni