TAASISI 141 ZAUNGANISHWA MFUMO WA GoVESB


MENEJA MAWASILIANO eGA SUBÌRA KASWAGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


Na Pilly Kigome- Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) tayari imeunganisha Taasisi 141 katika mfumo mkuu wa ubadilishanaji taarifa Serikali (GoVESB).

Ikiwa ndani yake kunapatikana mifumo ipatayo 148 na kati ya hiyo mifumo 109 inasomana na kupeana taarifa.

Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano eGA, Subira Kaswaga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.

Kaswaga amesema kuwa, mamlaka hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 10 ya mwaka 2019 ikiwa na jukumu kubwa la msingi ni kuratibu matumizi ya Tehema katika taasisi za Umma kuhakikisha taasisi hizo zinatumia Tehema kuhakikisha huduma za Serikali zinawafikia wananchi wa mijini na vijijini kwa njia ya kidijiti mahali walipo bila kuangalia mipaka ya mazingira.

Amesema mfumo huo ni daraja kati ya taasisi za Serikali na wananchi katika kuwasilisha changamoto na maoni yao mfumo huo umetambulika kimataifa kama ni jukwaa huru linalowasaidia wananchi kupata taarifa za serikali kwa wakati.

Aidha amefafanua mfumo huo madhubuti umeweza na kupata tuzo katika Umoja wa Mataifa wa ubunifu wa huduma za umma mwaka 2024 zilizotolewa nchini Korea.

“Katika kurahisha mifumo hiyo yote inatumika tunafanya jitihada mbalimbali ikiwa na pamoja na kukutana na taasisi za umma ambapo Julai 22 hadi 29 tunatarajia kukutana na taasisi zaidi ya70 za umma kwa lengo la kuwapa elimu kuhusiana na mfumo GoVESB” amesema.

Hata hivyo amesema taasisi zimekuwa na muitikio mzuri kadiri wanavyoangalia takwimu idadi ya taasisi zinaongezeka na idadi ya mifumo inayounganishwa katika mfumo huo inayobadilishana taarifa inazidi kuongezeka.

“Kama mamlaka jukumu letu ni kuhakikisha taasisi zote za umma zinaunganishwa katika mfumo huu ili kubadilishana taarifa” amesema Kaswaga

Aidha ameongeza eGA kuna kituo cha utafiti na ubunifu ya Tehema katika Serikali mtandao katika kituo hicho wanabuni mifumo mbalimbali ya Tehama ambayo italeta tija kwa serikali katika kurahisisha utendaji kazi na itasaidia utoaji wa huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijiti.

Kaswaga ametoa wito kwa taasisi za umma na wananchi kutumia kuwasilisha maoni na kero kupitia mfumo huo pamoja kufika kwa wingi katika ofisi husika kupata elimu zaidi kuhusiana na mifumo.


 

Chapisha Maoni

0 Maoni