RITA YAUPIGA MWINGI USAJILI WA VYETI MAONESHO YA SABASABA

 


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) wamesajili vyeti 4,567 katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Nipashe Ofisa Usajili RITA, Mariam Ling’ande amesema takwimu hiyo inaanzia toka maonesho yalipofunguliwa hadi kufikia Julai 9, 2024.

Ling’ande amesema katika idadi hiyo wamesajili vyeti katika maeneo tofauti ambapo vyeti vya kuzaliwa ni 4,326, ndoa 90, talaka 50, leseni za wafungisha ndoa tatu.

Wosia ulioandaliwa na kukamilika mmoja, elimu juu ya wosia 96 na udhamini mmoja.

Amesema wanaendelea na zoezi la kusajili na utoaji elimu kwa makundi tofauti yanayofika hapo.

“Natoa wito elimu juu ya wosia bado iko chini hivyo watu waje wapate elimu na waandike wosia tupo kwaajili yao” amesema

Kwa upande wake Ofisa Habari na Mawasiliano RITA GoodLuck Malekela amesema maonesho ya mwaka huu yamekuwa na uitikio mkubwa sana kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika kupata huduma.

Amesema wanaweza kupata urahisi wa kuhudumia uwingi huo kwakuwa huduma hizo zinatolewa kisasa kwa njia ya kidigitali na watu wanaweza kuondoka na vyeti vyao kwa wakati.

“Tunatoa wito watu waendelee kujitokeza kwa wingi tuko tayari kuwahudumia waje kwenye maonesho haya na waje wapate huduma zote muhimu na kuondoka na vyeti vyao” amesema.

Chapisha Maoni

0 Maoni