PURA YAPATA MWEKEZAJI MPYA MKOANI MTWARA ATAKAYEZALISHA FUTI ZA UJAZO MILIONI 100 KWA SIKU

MWENYEKITI WA BODI PURA HALFAN HALFAN AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WAHABARI


Na Pilly Kigome- Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) imesema imepata mwekezaji mpya mkoani Mtwara wa uchimbaji wa gesi asilia atakayezalisha futi za ujazo Milioni 100 kwa siku.

Mbali na hilo PURA imewataka wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kushiriki katika duru ya kutangaza maeneo ya uwekezaji wa petroli na gesi nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti waBodi ya PURA, Halfani Halfani leo Julai 11,2024 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 48 ya Sabasaba.

Amesema wana sababu za kuongeza wawekezaji kwakuwa kwa kipindi kirefu hawakuwa na wawekezaji katika maeneo mengi walikuwapo lakini maeneo hayo yamerudishwa serikali.

Amefafanua sheria ya mafuta inataka wawekezaji watafutwe kwa ushindani kwa kufanya mkutano wa kutangaza maeneo ya wawekezaji.

Amesema kwa kipindi kirefu walikuwa wanategemea gesi ya baharini katika maeneo ya Songosongo Kilwa na Mnazibay Lindi wanazalisha futi za ujazo milioni 250 kwa siku na kiasi kikubwa kinatumiwa kuzalisha umeme.

Ambapo asilimia 50 ya gesi hiyo inazalishia umeme na kiasi kingine kinatumika kwenye matumizi mengine.

Akifafanua majukumu ya PURA ni pamoja na kumshauri Waziri wa Nishati masuala ya mkondo wa juu wa utafutaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.

Jukumu la pili ni kusimamia ufanisi wa juu wa sekta kuhusu utafutaji gesi ili kujua gharama za utafutaji na wapi.

Pia wana jukumu la kuhakikisha Watanzania wanashiriki kwenye jukumu la utafutaji na uzalishaji wa gesi ikiwemo na kutunga sera ndogo za kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufaniisi na kusimamia uuzaji wa gesi nje ya nchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni