PURA NA MALENGO YA KUFIKIA NISHATI JAJIDIFU, MBIONI KUTANGAZA VITALU VIPYA PWANI

MKURUGENZI MKUU WA PURA MHANDISI CHARLES SANGWENI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAŔ ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema Tanzania imeweka malengo ya kutumia nishati jajidifu ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Mbali na hilo PURA ipo mbioni kutangaza vitalu vipya vya uchimbaji mafuta na gesi katika Ukanda wa Pwani hivi karibuni.

Mhandisi Sangweni ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea banda la mamlaka hiyo katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.

Amesema tayari wamefanya utafiti katika maeneo tofauti nchini kuwa asilimia 50 ya eneo lote nchini lina miamba tabaka yenye mafuta ambako maeneo hayo mengi yako Ukanda wa Pwani,Kati na Nyanda za Juu maeneo ya Mbeya.

“PURA iko mbioni kutangaza maeneo mapya ya uwekezaji nchini kwenye vitalu vya mafuta na gesi na tunashirikiana na wenzetu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),” amesema Sangweni.

Amesema katika kutangaza fursa hizo wataanza na Ukanda wa Pwani na kisha kuendelea maeneo mengine ukiwemo Singida na eneo la Kyela mkoani Mbeya.

Amefafanua katika mnyonyororo wa petrol wa kuongeza thamani zao la petrol kuna mikondo mitatu kuna mkondo wa juu ni wa kutafuta, kuendeleza na kuzalisha, mkondo wa kati ambapo petrol inapotoka katika mfumo wa tope unasafishwa na mkondo wa chini ambapo haya mafuta yanauzwa baada ya kusafirishwa.

“Katika upande wa ukuaji sekta nishati safi tunaenda kisasa zaidi tunaenda kutumia nishati inazuia uchafu wa mazingira(jajidifu) yenye malengo ifikapo 2060 dunia imefikia katika matumizi ya nishati jajidifu kwa kiwango kikubwa.

“PURA tuko hapa kushiriki maonesho haya ili kuendeleza kauli mbiu ya mwaka huu inayosema Tanzania ni sehemu sahihi kwa uwekezaji. Hivyo tunajenga mazingira bora ya wawekezaji” amesema

Chapisha Maoni

0 Maoni