Katibu Mtendaji wa PPAA James Sando
Na Mwandishi Wetu-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Rufani ya Zabuni za Umma(PPAA) imetengeza mfumo mpya wa kuwasilisha malalamiko kwa taasisi nunuzi na wazabuni katika ‘Moduli ya Usimamizi wa Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 48 Sabasaba, Katibu Mtendaji wa PPAA James Sando alisema mfumo huo umekuja mahususi kwaajili ya kuwasilisha malalamiko yote yahusuyo zabuni.
Alisema moduli hiyo imeweka sharti la lazima ambalo taasisi nunuzi na wazabuni wote lazima wawasilishe malalamiko hayo kwa njia ya kielektroniki wa Nest kinyume na hapo malalamikoyako hayatapokelewa.
Sando alibainisha sheria hiyo imekuja kuwasaidia watanzania katika mchakato mzima wa ununuzi wa umma katika mashauri yanapoanza hadi pale yanapokamilika.
“Lengo la mfumo huu mpya wa NeST utamrahishia mnunuzi kuepuka gharama ambazo si lazima katika kuwasilisha malalamiko popote alipo ataweza kuwasilisha”.Pia mfumo huo umekuja kutokana na mabadiliko yaliyotokea na kuboresha mwaka 2023 na kuanza kutumika Juni 2024.
Dhima ya Mamlaka kutatua migogoro ya wazabuni inayotokana na mchakato wa ununuzi wa umma kwahaki na kwa wakati ili kuhakikisha uzingatiaji wa sheria inayosimamia ununuzi wa umma.
Alisema majukumu makubwa ya mamlaka ni pamoja kupokea malalamiko na rufaa zitonazazo na michakato ya ununuzi wa umma, kufanya mapitio ya maamuzi ya maafisa masuuli kuhusiana na michakato ya ununuzi wa umma.
Kufanya mapitio ya waamuzi wa kuwafungia wazabuni uliofanywa na Mamlaka ya udhibiti ununuzi wa umma ikiwemo na kuagiza hatua za kuchukua ili kurekebisha pale inapoonekana kuna ukiukwaji wa taaratibu za kisheria katika michakato ya ununuzi.
Kuruhusu hatua za marekebisho kuchukuliwa pale ambapo itabainika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu katika mchakato wa ununuzi.
Khamisi Mbaga aliiambia Nipashe kuwa PPAA na mfumo wa NeST utawasaidia Watanzania wengikatika kuwasilisha malalamiko hayo kutofautisha na awali

0 Maoni