NJOONI UDOM MUANDALIWE MUENDANE NA SOKO LA DUNIA" PROF.KUSILUKA

PROF.LUGANO KUSILUKA AKITEMBELEA MABANDA YA UDOM KATIKA VIWANJA VYA SABASABA


Na Pilly Kigome- Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lugano Kusiluka amesema wanajikita kutoa wataalamu wabobezi ili kuendana na soko la dunia.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam katika meonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Prof.Kusilika amesema UDOM wanawasuka wasomi katika nyanja zote kwakuwa sasa hivi mamboyote yanaendeshwa kisasa ikiwemo hata kuandaa wafanyabiashara wasomi watakaoendana na soko la kimataifa.

Amesema ushiriki wao katika maonesho hayo ikiwa na pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali zinazofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza na kuijenga nchi.

Amesema ushiriki huo utaleta tija kwani bunifu zao zitaonekana na mataifa mbalimbali na kukitangaza chuo kwa ujumla ikiwa na pamoja na kuvutia watu wengi kujifunza na kutambua kozi mbalibali zinazopatikana katika chuo hicho.

Amefafanua watu wengi wamekuwa wakivutiwa na banda hilo kwakuwa wameonesha umahiri mkubwa unaofanywa na wakufunzi na wanafunzi katika tafiti na bunifu mbalimbali.

“Tumefurahi tumetembelewa na wanafunzi wetu zaidi ya 300 waliyohitimu miaka ya nyuma na kuja kutupa mafanikio na walivyopokelewa katika ajira zao” amesema

Chuo hicho kinatoa waalamu wengi ikiwemo sanaa, lishe, Tehama, ufugaji wa samaki, tekolojia za habari na zingine nyingi.

Pia alitoa wito kwa wanafunzi na watu wanaotaka kujiendelea kujiunga na chuo hicho kuleta tija na kujiongezea ajira na kujiajiri. 

Chapisha Maoni

0 Maoni