MWENYEKITI SALMIN AAHIDI KUTATUA KERO ZA WAKAZI ZA WAKAZI WAKE

ABDALLAH SALMIN MWENYEKITI SERIKALI MTAA KARIAKOO MASHARIKI

Dar es Salaam

Na Pilly Kigome

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Kariakoo Mashariki Abdallah Salmini ameahidi kutatua kero zinazowakabili wakazi wa mtaa huo ikiwemo ya barabara ya mtaaa wa Mchikichi.

Hayo ameyasema leo katika mkutano wa hadhara wa kuwasilisha ilani ya miaka mitano yaliyofanyiwa kazi ya Chama uliofanyika makutano ya barabara ya LivingStone na Mchikichi jijini Dar es salaam.

Salmin amesema jukumu lao kubwa ni kuhakikisha kero zinazowakabili wananchi zinatatuliwa kwa vitendo.

Amesema moja ya changamoto inayowakabili wakazi wa mtaa huo ni barabara ya mtaa wa Mchikichi inasumbua kwa muda mrefu kutokana na makubaliano ya Serikali ya mkandarasi yalikuwa hayajakamilika kuanza ujenzi wa barabara hiyo.

Changamoto ingine ni wamachinga kuweka meza zao nje maduka ambayo kwasasa wanashughulikia kila mmoja aweze kufanya kazi zake bila kumbughudhi mwenzie.

Katika mkutano huo pia waliweza kutambulisha timu ya ulinzi shirikishi kwa wananchi wa mtaa huo.

“Tunamshukuru Mbunge amechukua kero zetu na ameahidi kwenda kufanyia kazi, kwakuwa ametuahidi ujenzi wa barabara utaanza mwezi ujao(AGosti)” amesema


 

Chapisha Maoni

0 Maoni