MAKALLA AIPA KONGOLE SGR

KATIBU MWENEZI CCM TAIFA AMOS MAKALLA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KITUO CHA TRENI SGR JIJINI DAR ES SALAAM


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Amos Makalla amewataka Watanzania kuiamini Serikali yao hasa wanapoambiwa imekopa fedha hizo zinakwenda kwenye miradi yakutanua maendeleo ya nchi na si vingine.

Hayo ameyasema leo Julai 13, 2024 mara baada ya kuwasili katika kituo kikuu cha reli ya kisasa (SGR) km ziro jijini Dar es Salaam  akitokea mkoani Morogoro kwa kutumia usafiri huo.

Amesema  mradi huo wa reli ya kisasa umejengwa kwa kiwango cha juu hivyo Watanzania wanatakiwa kutambua wanapoambiwa serikali imekopo wapeleke jicho lao kuangalie miradi hiyo ya kimkakati na maendeleo na mafanikio yanayopatikana nchini.

Amefafanua gharama iliyotumika kujengea reli hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ni dola Bil 1.2 na kutoka Morogoro hadi Dodoma ni dola Bil 1.9 jumla ni dola Bil. 3.1 ujenzi kukamili.

“Watanzania wanatakiwa waelewe na kutambua ni wapi tumetoka, tuko wapi na tunaenda wapi watatambua kazi na juhudi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza na kukamilisha mradi huu mkubwa aliouacha Marehemu John Magufuli” amesema Makalla

Juzi tulikuwa na mjadala bungeni kuhusu deni la Taifa, kupitia reli watanzania wataona ni jinsi gani mkopo umefanya kazi kwa kuweka miundombinu rafiki ya  kuchochea uchumi na kuongeza mapato kwakuwa wataliii wengi wanautimia usafiri huo.

Abiria aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Yusuph Mwinyi mkazi wa Dodoma amesema kwa kupitia usafiri huu wa reli ya kisasa SGR Serikali imefanya kitu kikubwa na watanzania wengi kuuamini na kuupokea usafiri huo.

Amesema usafiri huu unaokoa muda ukitofautisha na basi kwani waliweza kutoka Morogoro saa 12:20 asubuhi na walifika Dar es Salaam saa 1:50.

“Mimi nilidhani ni porojo kumbe ni kweli kabisa tumesafiri kwa raha na amani na kutumia muda mfupi tofauti na ninavyotumia usafiri wa basi” amesema

Chapisha Maoni

0 Maoni