MAGARI 5000 YANATUMIA GESI- EWURA



Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk. James Mwainyekule amesema hadi sasa magari 5000 yanatumia gesi.

Na hiyo imesaidia kwa asilimia kubwa kupunguza dola kutumika katika0⁰⁰ kuagiza mafuta nje, kwa sababu gesi hii ya mafuta inatoka nchini.

Amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali hadi kufikia sasa Juni 30, mwaka huu ubora wa mafuta nchini uliimarika na kufikia asilimia 97.

"Tunazingatia bei katika soko la dunia tukifuatilia na kila mwezi bei zilishuka na kupanda kulingana na soko la dunia". amesema

Akifafanua kuhusu majukumu ya EWURA kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya ni pamoja na kutekeleza kazi zote zilizoanishwa kwenye sheria ya EWURA na Sheria za Kisekta. 

Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni, Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma, Kudurusu na kusimamia bei za huduma.

Kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro, Kutoa taarifa kuhusu kazi za udhibiti.pamoja na Kupata maoni ya mamlaka zingine za kiudhibiti na Kusimamia utekelezaji wa Sura Na 414 ilyoianzisha EWURA.

Dk.Mwainyekule amesema mwezi uliopita walisaini mkataba na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupima utendaji kazi na namna ya utekelezaji wa kazi

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Nishati Felchesmi Mramba amesema kwenye eneo la nishati wanadhibiti umeme, gesi asilia.

EWURA wamedhibiti ubora na umeme upatikanaji wa huduma umeboreka nchi yetu ni miongoni zenye bei za chini sana ya huduma za umeme ukilinganisha na majirani zetu.

"Huduma umeimarika na siku za hivi karibuni nyinyi ni mashahidi kule kukatika kwa umeme umepungua na katika gesi asilia EWURA imesaidia sana" amesema



Chapisha Maoni

0 Maoni