KATAVI KUNUFAIKA NA MRADI WA UMEME WA BIL116

 


Na Mwandishi Wetu -Nifahamishe News Blog

KAMPUNI ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (EDTCO) imesema inajipanga kutekeleza mradi wenye thamani ya Sh.Bilioni 116 wa kusambaza umeme Mkoani Katavi. 

Hayo yamesemwa Julai 9,2024 na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi EDTCO Dismas Masawe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Massawe amesema EDTCO imejipanga kuhakikisha inakamilisha miradi mbalimbali ya usambazaji umeme nchini inakamilika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25.


Amesema tayari wameshaunganisha umeme zaidi ya vijiji 130 vilivyopo Mkoani Mbeya ambapo umegharimu zaidi ya Bilioni 50 ambapo Wanatarajia kumalizia kusambaza Umeme katika Vijiji 30.

Kwa Upande wake Meneja wa Fedha EDTCO CPA Mnyembi amesema kila mwaka kiwango cha fedha kinaongezeka katika kampuni hivyo mwaka huu 2024 wanatarajia kupata zaidi ya shilingi Bilioni 90 katika mapato.

Chapisha Maoni

0 Maoni