KAIMU MKURUGENZI WA UCHUNGUZI WA BIDHAA NA MAZINGIRA (GCLA) SHIMO PETER
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SAĹAAM
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imebainisha upimaji wa sampuli ya DNA unatumika katika nyanja nyingi katika kupata majibu sahihi na kuondoa utata katika kesi husika..
DNA ni zaidi kubaini uhalali wa mtoto bali hutumika katika utambuzi wa wanyama na binadamu katika majanga kama ajali ikiwemo na kutambua jinsi ya mtoto kwa wale wanaozaliwa na jinsia tata.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Kurugenzi za Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (GCLA) Shimo Peter katika maonesho ya 48 ya Sabasaba katika banda hilo.
Amefafanua Mamlaka ya MkemiaMkuu wa Serikali ina majukumu yamegawanyika katika makundi makuu matatu ikiwemo uchunguzi wa sampuli za kimaabara, uchunguzi wa sampuli za mazingira na uchunguzi sampuli usalama mahala pa kazi.
Amesema watanzania wanatakiwa watambue kuna chunguzi zaidi zingine za vinasaba vya DNA zinatumika katika matukio ya jinai, matukio ya sumu ikiwemo na uhalifu.
“Watanzania waje wajitokeze kwafike katika banda letu kupata elimu na kujifunza ikiwemo kupata ushauri na kujioneakazi zinazofanya na mkemia mkuu wa serikali” amesema
Awali Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelice Mafumiko amesema kuna ongezeko la sampuli zilizofanyiwa uchunguzi ambapo kwa mwaka 2021/22 sampuli 155,817 zilichunguzwa sawa na asilimia 139.94 la lengo la kuchunguza sampuli 111,349
Kwa mwaka 2022/23 sampuli 212,306 sawa na asilimia 133.9 ya lengo la kuchunguza sampuli 158,600 zilizofanyiwa uchunguzi wa kimaabara.



0 Maoni