FIKENI KIJIJI CHA.BIMA SABASABA KUPATA ELIMU CHANGAMOTO ZA BIMA

 


Na Pilly Kigome-. Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

MSULUHISHI wa Migogoro ya Bima, Margaret Mngumi amesema wanatumia Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kusuluhisha changamoto za bima na kutoa elimu zinazohusiana na bima.

Migogoro hiyo ikiwemo ile ya viwango vya fidia ya bima tafsiri sahihi ya mkataba wa bima, mara nyingi mteja na kampuni ya bima wanakuwa hawaelewani kuhusiana na tafsiri hizo

Ameyasema hayo Julai 7,2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari, amesema wa habari katka maonesho ya 48 ya Sabasaba.

Amesema wanatumia maonesho hayo kutoa elimu na kusuluhisha migogoro kutoka kwa wadau mbalimbali na kuwataka wananchi kutembelea Kijiji cha Bima kilichoko ndani ya maonesho hayo ambako kuna banda la msuluhisi wa migogoro hiyo. 

Mwakilishi wa Kampuni za Bima zinazoshiriki maonesho hayo, Alilya Kwayu, amewashauri Watanzania kujenga utamaduni wa kukata bima kama za afya, nyumba, magari, elimu, maisha ili iwe ziwasaidie pindi wanapopata majanga mbalimbali.

Kwa upande wake Meneja Uandikishaji kutoka Kampuni ya Bima Mtawanyo (Grand Reinsurance), Charles Chanya, amesema wanatoa huduma kwa makampuni ya bima kwa lengo la kuyaongezea uwezo katika shughuli zao za kila siku. 

“Kampuni za bima huwa zinafanya biashara ambazo pengine inaweza kufikia hatua zinazidi uwezo, yanapozidiwa uwezo yanakuja katika kampuni za bima mtawanyo kuomba kuongezewa uwezo ili kuandikisha bima zaidi, tunaongeza uwezo wa kifedha lakini hatuwapatii fedha, wanaandikisha bima kwa kutumia mtaji wetu,” amesema Chanya.


 



Chapisha Maoni

0 Maoni