Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imewataka Watanzania wajikite kwenye matumizi ya gesi kwenye magari kuendena na teknolojia ikiwemo kupunguza matumizi ya fedha.
Katika ripoti ya gesi asilia EWÚRA wanawahamasisha wenye magari warekebishe gari zao ili watumie gesi asilia iliyobanwa (CNG).
Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA Titus Kaguo leo Julai 5 katika maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), kwenye banda hilo.
Amesema katika banda hilo kuna ripoti mbalimbali za utendaji wa sekta ya umeme, maji, petroli na ile ya gesi asilia.
"Wale wanaotaka kuwekeza tutawaambia wawekeza katika vituo vya gesi asilia iliyokandamizwa Tanzania inawezekana," ameeleza.
Amesema Shirika la Viwango Tanzania (TBS), tayari lilishafanya marekebisho ya viwango vya ubora ambapo kituo chochote Tanzania kinaweza kuweka mradi wa ufungaji wa mifumo ya gesi asilia (CNG).
Amefafanua kuwa ili CNG iweze kutumika nchi nzima itaenda kwa kusogea tofauti na bidhaa nyingine na kwamba hilo wazo ni la wizara kwamba EWURA ichukue kama chanzo kingine cha matumizi ya nishati mbadala kutokana na hali mafuta duniani.
Kaguo amesema kuwa katika banda hilo wataalam wote wapo wa gesi asilia, sekta ya maji bili mbakikizi, petroli, leseni huku akisema wamejipanga na kuhamasisha kila changamoto inatatuliwa.
Ameeleza kuwa hata alivyokuwa akizindua ripoti za taarifa za utendaji wa nishati moja ya taarifa zake amesema anataka taasisi zitoe taarifa kwa Umma ili watanzania wajue wizara inachokifanya.
" Kuna kina mama wamefika hapa wanataka kuungiwa gesi na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), tumewaelekeza kinachotakiwa lakini tumewaelekeza waende TPDC ili waweze kuelewana na kuungiwa gesi na hii inakuwa ni majibu ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ambaye anataka Tanzania iwe ni moja ya nchi bora kwenye suala la nishati safi ya kupikia.
Ameongeza kuwa EWURA ipo chini ya wizara hiyo na kwamba wapo katika maonesho hayo kutoa taarifa kwa Umma majukumu ambayo wanayafanya yakiwamo ya kudhibiti Petroli na bidhaa zake, umeme na gesi asilia, maji na usafi wa mazingira.
Ameeleze kuwa watanzania wengi wamekuwa wakipatiwa elimu ya kutosha huku akisema watu waliofika katika banda hilo ni wale wenye shauku ya kuwa na leseni ya umeme.
Amesema wizara iliipatia EWURA mamalaka ya kutoa leseni ndogo za ukandarasi zenye madaraja mbalimbali huku akieleza kwamba leseni hizo zipo kwenye mtandao.


0 Maoni