CRDB INSURANCE MKOMBOZI WA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI

 

NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA AKISAINI KITABU CHA MAHUDHURIO ALIPOTEMBELEA BANDA LA CRDB INSURANCE


Na PillyKigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Jumanne Sagini ameitaka Benki ya CRDB kutoa elimu zaidi kuwafikia wananchi kuhusiana na Bima ya Mifugo na Kilimo.

Maagizo hayo ameyatoa Julai 5, 2024 alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya 48 ya Tantrade jijini Dar es Salaam.

Mh.Sagini amesema bima hiyo ni muhimu kwa watanzania wote hususani wakulima na wafugaji kwani imekuja kuwakomboa makundi hayo.

Amesema wananchi wakijua kuweka tahadhari kuhusiana na majanga yasiyotarajiwa wananchi watafaidika kwa kiasi kikubwa kwani bima hiyo itamjali na kumlinda.

“Mkazane kutoa elimu hasa pembezoni mwa miji kwa wananchi ili waweze kuchukua bima kuwalinda na majanga yasiyotarajiwa” ameagiza Sagini

Kwa upande wake Anjelina Kimweri Afisa Mauzo CRDB Insurance amesema bima hizo ni kubwa kwa sasa kwa upande wa bima imekuja kuwakomboa wafugaji na wakulima.

Amefafanua bima ya kilimo inamlinda mteja kutokana na ukubwa wa shamba baada ya kufanyiwa tathimini na kulinda mazao yake kutokana na majanga ya ukame, mafuriko, mazao kuliwa na wadudu shambani bima hiyo itamlinda.

Amesema kwa upande wa mifugo bima itamlinda mteja kutokana na magonjwa yasiyotarajiwa, vifo na majanga mengine yatokanayo na wanyama.

Amesema wanakuja na teknolojia mpya ambayo itatambua mfugo wowote iwe, mbuzi, ng’ombe kwa kutumia pua.

CRDB Insurance ilizinduliwa May 2023 na tayari imeshaanza lkuwanufaisha wafugaji na wakulima katika baadhi ya mikoa nchini.

Chapisha Maoni

0 Maoni