CHUO USTAWI WA JAMII YANADI KOZI YA.MALEZI NA MAKUZI KWA MTOTO


Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

DAR ES SALAAM

CHUO cha Ustawi wa Jamii kimeanza udahili wa mtaala mpya ya malezi na makuzi ya mtoto ili kuleta tija kwa maendeleo yao.

Hayo yamesemwa na Afisa Mkuu wa Chuo hicho Dk.Joyce Nyoni wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 48 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Dk.Nyoni amesema mtaala huo mpya mahususi unakwenda kuwasuka wakufunzi na wataalamu wa kwenda kufundisha walimu wa watoto, walezi wa watoto ikiwemo wale wenye vituo vya kulelea watoto ikiwemo yatima na vituo vya daycare na makundi mengine yahusuyo watoto.

Amesema mtaala huo utatolewa kwa ngazi ya Cheti na Diploma katika Kampasi ya Kisangara Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Aidha amefafanua kozi hiyo itakwenda kutoa suluhisho kusaidia kuweza kuwajenga kuhusiana na malezi ya watoto kwani jamii inakabiliwa na changamoto kubwa katika malezi hayo ikiwemo kuwepo kwa ukatili kwa watoto.

“Tunaona jamii inavyokabiliwa na changamoto hasa za ukatili kwa watoto, ikiwemo na changamoto za malezi pia, hivyo kozi hii inakuja kuwajenga walimu wa walimu ikiwemo na kuja kuongeza ajira” amesema Nkwao

Mtaala huo utakwenda kuwaongoza katika ulinzi wa mtoto, kuwafundisha taratibu za kuwaongoza katika michezo ya watoto, saikokojia ya mtoto, sanaa na vingine vingi vinavyohusu makuzi ya mtoto kwa ujumla.

Amefafanua tayari Chuo kimeshanza kudahili wanafunzi hivyo kuwataka Watanzania kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kwenda kujiunga na kozi hiyo muhimu katika ustawi wa mtoto.

“Watanzania, wanafunzi wenye uhitaji a kutaka kujiunga kozi hii waje wajitokeze kwenye banda letu hapahapa kwenye banda letu tunafanya usasajili” amefafanua

Chapisha Maoni

0 Maoni