ARUSHA MATTRESS COMPANY YAJA NA MAGODORO YANAYOSAIDIA KUTENGENEZA AFYA


Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM

WATANZANIA watakiwa kutambua ubora wa magodoro wanayotumia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo mgongo na pingili.

Hayo yamesema na Afisa Mauzo kutoka Arusha Mattress Company Limited Richard Kaduma katika maonesho ya 48 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Kaduma amesema kuwa watanzania wanatakiwa kutambua ubora na viwango vya magodoro wanayoyatumia ili kuepukana na changamoto za kiafya.

Amesema magodoro yatokanayo na kampuni ya Arusha Mattress yana ubora wa kipekee na yana uwezo ya kumlinda mtumiaji kupata usingizi mzuri.

Amesema magodoro yatokanayo na kampuni hiyo yanafanya mtumiaji kuepUkana na magonjwa ya afya ya akili kwa kuwa linampatia mtumiaji usingiziri mzuri na afya ya akili inakaa vizuri.

Amesema wana magodoro ya aina zote yenye vitambaa vigumu na laini kwa matumizi ya makundi yote ikiwemo wazee, wagonjwa na watoto.

Aidha amesema katika msimu huu wa Sababasaba wametoa punguzo la asilimia 10 hadi 14 watakaoweza kufika na kununua godoro katika banda hilo ndani ya viwanja hivyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni