Na Maandishi Wetu-Nifahamishe News Blog
DODOMA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba kujadili mambo muhimu yakiwemo mifumo yĆ mafao.
Viongozi hao wamekutana leo Juni 28,2024 Mkoani Dodoma baada ya kuhitimisha Bunge.
Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA.
Aidha Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali maslahi ya watanzania.
Pamoja na hayo Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.


0 Maoni