Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamuhuri ya Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu kuanzia June 21 hadi 23 ikiwa ni pamoja kuja kujifunza katika mradi wa reli ya kisasa (SGR) uliopo nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje Balozi Dkt.Samweli Shelukindo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Balozi Shelukindo amesema Rais huyo ambae ni Mwenyekiti wa sasi viongozi Afrika katika kudhibiti malaria ALMAA ujio wake utaleta faida kubwa kunufaika kwa Tanzania.
Amesema lengo la ziara hiyo ni kukuza na kuimarisha mahusisano ya kidemokrasia, Ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili ikiwemo na kuibua maeneo mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ushirikiano katika uzalishaji wa korosho.
Kushirikiana katika kudhibiti ugonjwa wa malaria ambapo Sektetariate yake iko hapa Tanzania, ikiwemo na kuinua viwango vya ufanyaji biashara, uwekezaji kupitia eneo huru la biashara Barani Afrika ambalo Tanzania imesaini na kuridhia.
“Kwa kupitia fursa hii soko limefunguka hivyo tutaweza kujua ni bidhaa gani ambazo wafanyabishara wetu wanaweza wakauza katika nchi hiyo” amesema Balozi.
Tanzania imejipanga kunufaika kwa kuzingatia ziara hiyo itatoa fursa kujadili maswala mbalimbali ya uwekezaji na mashirikiano ya kibiashara.

0 Maoni