MUHAS YATARAJIA KUTOA MATOKEO YA TAFITI ZA KISAYANSI KATIKA KONGAMANO LA 12 MLOGANZILA

PROF. APPLINARY KAMUHABWA NA MKURUGENZI WA TAFITI MUHAS DKT.NAHYA SALIM WAKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM


DAR ES SALAAM

Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kinatarajia kufanya kongamano la 12 la kisayansi litakalowakutanisha zaidi ya wajumbe 400 ikiwa na pamoja na kumuenzi Mkuu wa Chuo hicho wa kwanza Hayati Dkt.Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Tanzania.

Kongamano hilo la siku mbili litaanza June 27 hadi 28, 2024 linatarajiwa kufanyika katika kituo cha Afrika Mashariki Cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu, MUHAS Kampas ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Makamu Mkuu Chuo Kikuu Shirikishi Muhimbili (MUHAS)Prof.Appolinary Kamuhabwa wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

Prof. Kamuhabwa amesema dhumuni la kongamano hilo ni kushirikishana, kuelezana, kujifunza na kubadilishana ujuzi unaotokana na matokeo ya tafiti zinazofanywa kutumika na watekelezaji, wadau, wafanyakazi wa huduma za afya ikiwemo kusambaza ufanisi wataalamu.

Pia Chuo kitaonyesha matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni za ndani na nje ya nchi ikiwemo kubadilishana mawazo kwa wataalamu kutoka nchi nyingine duniani ikiwa ni kuboresha afya kupitia tafiti.

Katika kongamano hilo tafiti za kisayansi 80 zitawasilishwa kwa njia ya maongezi na tafiti 107 zitawakilishwa kwa njia ya mabango.

Amesema tafiti hizo zikiwemo magonjwa yasiyoambukizwa Afya ya Akili,Upasuaji na Lishe. Magonjwa ya kuambukiza na usugu wa vimelea Jicho,Sikio, Pua na koo.

Afya ya mama, mtoto mchanga, mtoto na vijana rika, utafiti wa mifumo ya afya, tiba mbadala za asili, uvumbuzi wa dawa maendeleo ya chanjo na masuala mtambuka maadili na taaluma, akili ya bandia, teknolojia na afya ya kazini.

Mkurugenzi wa Tafiti Machapisho na Ubunifu Dkt.Nahya Salim amesema baadhi ya matokeo ya tafiti zitakazowasilishwa ni pamoja na kugundua asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU wana kiwango cha juu cha sukari unaosababishwa na unywaji wa pombe na shinizo la juu damu.

Utafiti ulifanywa Kinondoni umegundua asilimia 54.5 ya wanawake wanatumia vipodozi vya kujichubua ambao wengi wanaotumia vipodozi hivyo ni wale wanaofanya kazi mapokezi.

Upatikaji wa huduma za wodi maalum za kulaza watoto wachanga ni asilimia 48

Chapisha Maoni

0 Maoni