MAHUJAJI 3300 WAAGWA BAKWATA, WAKUMBUSHWA KUIOMBEA NCHI


Na Bakari Ezekiel

MAHUJAJI 3300 kutoka Tanzania Bara wanatarajiwa kuondoka kwenda nchini SaudArabia Mji wa Makka kwaajili ya kwenda kuhiji kutimiza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu.

Mahujaji hao wanatarajiwa kuondoka kwa nyakati tofauti kuanzia leo ambao wameagwa makao makuu ya Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuwaaga mahujaji hao kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa Shekhe Hamid Masoud Jongo amewataka na kuwakumbusha mahujaji hao kwenda kuiombea nchi na kuwaombea viongozi wakuu nchini kuliendesha Taifa kwa weledi ikiwemo kuliombea Taifa amani na utulivu uliopo uendelee kudumu.

Shk.Jongo amewausia mahujaji hao wanapokwenda huko wafate kinachowapeleka huko na wafate sheria na kanuni ili waweze kutimiza malengo yao yanayowapeleka huko na si kuchukulia kama wanaenda kutalii.

Mkurugenzi wa Hijja Bakwata Taifa pia Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi za Hijja Tanzania Bara 2024/1445H Shk. Haidary Kambwili amesema mahujaji hao wanaosafiri ni wale waliotumia taasisi 13 zilizoungana pamoja kwaajili ya kusafirisha mahujaji wameungana kuanzia mwakahuu na wameona wawaage mahujaji hao kwa pamoja ili kuweza kuleta mshikamano na umoja pindi mahujaji wanapokuwa mji huo tukufu.

Amesema mwaka huu uitikio wa wanawake kwenda kuhiji umekuwa mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita hiyo inaonyesha muamko kwa kundi hilo.

Hata hivyo amesema katika kusafirisha mahujaji hao walikutana na changamoto kadhaa ikiwemo kukosa usawa kati ya bara na Zanzibar katika baadhi ya vipengele katika utoaji huduma hizo za kusafirisha mahujaji na kuomba kuwe na usawa katika hilo.

Mbali na hilo amesema walikutana na changamoto ya ukosefu wa dolalakini ilikuwa ni tatizo la kidunia lakini Serikali na taasisi muhimu kama mabenki imeweza kusaidia na mahujaji hao wanaweza kusafiri.

Chapisha Maoni

0 Maoni