Na.Pilly Kigome
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Kariakoo inaelekea kufanya mkutano Mkuu June 13 kwaajili ya kutoa Mrejesho wa mambo waliyotekeleza na yasiyotekelezwa Serikali katika changamoto zao walizowakilisha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo June 7, 2024 Mwenyekit i wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Martin Mbwana amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwakutanisha katika kikao kazi na Mawaziri watatu akiwemo Waziri wa Fedha, Uwekezaji na Mambo ya ndani kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili
Amesema wameiomba Serikali wawashirikishe katika changamoto kubwa zinazowakabili za ukosefu wa ushirikishwajì kwa wadau muhimu wakiwemo FCC,TRA na JIJI kwani kufanya hivyo kunakuwa na wimbi la vishoka.
Hatahivyo
wanaiomba serikali iingilie kati sakata la kikodi na risiti za EFD.
Mbali na hayo pia wameiomba Serikali iangalie wafanyabiashara wa kati na wa chini Rais anapokwenda katika ziara zake za nje ya nchi.
Kwaupande wake Msemaji wa Jumuiya hiyo Mast Mgeni amèsema wanaiomba serikali iangalie kwa jicho la huruma kuwaangalia zaidi wafanyabiashara wazawa na kati katika jengo la biashara la kimataifa la Soko la Ubungo.
"Wafanyabiasharanwa.kichina wamekuwa wakifanya biashara kuwangusha wazawa kwa kuuza bidhaa kwa bei ya chini jambo ambalo si sawa" amesema

0 Maoni