Na.Mwandishi Wetu-Nifahamìshe News Blog
DAR ES SALAAM
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Allience for Democratic Change, ADC, Hamad Rashid kung'atuka katika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba, Hassan Doyo ameibuka kuwania kiti hicho.
Doyo ambaye alikuwa Katibu wa Chama hicho, ametangaza kuwania nafasi hiyo leo, Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam na kujinasibu kuwa anazo sifa za kukalia kiti hicho.
"Sababu kubwa ambayo imenifanya kuwania nafasi hiyo ni kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha baada ya kulelewa vema na aliyekuwa Mwenyekiti wetu, Hamad Rashid.
"Nimekaa na Mwenyekiti wetu kwa muda wa miaka 10 nikiwa Katibu Mkuu na sikuwahi hata siku moja kutofautiana naye na nimejifunza mengi ikiwemo suala uvumilivu na kuheshimu Katiba, ambayo ameitekeleza kwa vitendo kwa kuondoka madarakanj kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea," amesema.
Ameongeza kuwa ikiwa atafanikiwa kushika nafasi hiyo, moja ya mikakati yake ni kukiimarisha chama kiwe kikuu cha upinzani na kifanye vizuri bungeni na kuisimamia vema Serikali maslahi ya Watanzania.
Pia wakati akitangaza kuwania nafasi hiyo aliambatana na anayegombea umakamu uenyekiti, scolastica Kahana aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Kibaha Mjini katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Tofauti na hilo, Doyo ametoa wito kwa wana siasa ambao wameshindwa kwenye chaguzi wa ndani ya vyama kujiunga na ADC ili kuongeza nguvu ya kufanya vema kwenye chaguzi, zijazowa Serikali za Mitaa Oktoba mwaka huu na uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani.
"Ni vizuri hata ndigu yetu Peter Msigwa ambaye amshindwa kwenye uchaguzi wa ndani wa chama, kama itampendeza anaweza kujiunga kwetu na ninaamini atatuongezea nguvu kubwa kwenye ushindani wa siasa ya vyama vingi," amesema.
0 Maoni