Na Pilly Kigome-Nifamishe News Blog
DAR ES SALAAM
MAY 25 mwaka huu Tanzania inakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika ikiwa na pamoja na kuadhimisha miaka 20 toka kuanzishwa kwa Baraza hilo May 2004.
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mkutano huo ambao utahudhuriwa na wanachama kutoka nchi 15 za Afrika utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) wa jijini Dar es salaa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba ameviambia vyombo vya habari kuwa, katika mkutano huo kutakuwa na mada mahususi ambapo kila wiki kutakuwa na dhima mahususi katika kipindi hicho cha mkutano.
Amefafanua wiki ya kwanza kutajadiliwa maswala ya usuluhishi, wiki la pili watajadili misaada na mahitaji ya binadamu, wiki la tatu watajadili nafasi ya usalama wa wanawake na vijana na ya nne watajadili misheni za amani.
Pia siku hiyo kutakuwa na jopo mazungumzo na majadiliano kuhusiana na hali ya ulinzi na usalama kuhusu hali ya Afrika kwa miaka 20 iliyopita na muelekeo kuhusiana na miaka ijayo na Jopo hilo litasimamiwa na viongozi maraisi wastaafu wa Afrika.
Mh.Makamba amesema Tanzania imekuwa na historia adhimu ya tukio hilo kwakuwa imekuwa ni kitovu cha kukomboa nchi nyingi za Afrika kupigania Uhuru Barani Afrika waliitumia Dar es Salaam kama sehemu ya kujipanga na kupigania uhuru huo na vyama vingi vilianzishwa jijini humo ikiwemo chama cha Flerimo pamoja nchi zingine zikiwemo Namibia, Zimbabwe, Msumbjiji walikaa muda mrefu kujipanga kutafuta uhuru wa nchi zao.
Mh. Makamba amefafanua zaidi kazi ya Baraza hilo linakuwa na wajibu wa kusimamia migogoro isitokee Afrika, pia kusimamia migogoro pindi inapojitokeza.
“Hivyo kutokana na umuhimu wa chombo hicho, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa miaka 20 iliyopita, na kutokana na umuhimu wa kuwa na chombo imara basi kuna umuhimu wa kuadhimisha sherehe kubwa hapa Tanzania tukiwa kama wenyeji wa Mwezi May”. amesema
Katika Baraza hilo la Afrika kuna kuwa na utatu ambapo kunakuwa na vikao vya maraisi, mawaziri, na mabalozi unaokutanisha nchi wanachama ambapo kunakuwa na mzunguko wa uenyeji wa vikao hivyo.



0 Maoni