DAR ES SALAAM
Na Pilly Kigome-Nifahamishe News Blog
MABALOZI wa nchi Huru za Umoja wa Afrika wanatarajia kufanya Maadhimisho ya miaka 61 ya Umoja huo kwa kuweka mikakati katika kuwekeza katika elimu ikiwemo na kufanya riadha.
Mbali na hilo wataadhimisha siku hiyo kwa kula chakula cha pamoja pamoja na kutembelea shule zenye uhitaji maalum za jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Bujiku wakati akizungumza na waandishi wa habari Wizarani hapo.
Amesema kuwa maadhimisho hayo yamekuja na sura mpya ya kuwekeza kwenye elimu kwaajili ya maendeleo ya Afrika.
Amefafanua mabalozi watatoa misaada kwenye shule nne zenye mahitaji maalum ikiwemo Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko,Shule ya Secondari Pugu, Jeshi la Wokovu na Shule ya Sekondari Jangwani.
Vilevile maadhimisho hayo yatakua na kupata chakula cha pamoja May 25 kwaka huu katika Hotel ya Serena ya jijini Dar es Salaam.
Katika maadhimisho hayo mbio za riadha zitaongozwa na mabalozi ambapo kutakuwa na umbali wa km 5 hadi 15.
Akizungumza kwa niaba ya mabalozi Balozi wa Comoro Dk,Ahmada El Badaoui Mohamed alisema wamekuja na mikakati hiyo ikiwa pamoja na maadhimio ya kutaka kuboresha elimu ya bara la Afrika.
0 Maoni