Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
TAASISI ya Vijana Light of success imewajengea uwezo wa elimu za biashara zaidi ya wanawake 100 Mburahati ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
MKURUGENZI WA TAASISI YA VIJANA LIGHT OF SUCCESS ZENA MULOKOZI AKIZUNGUMZA NA WANAWAKEMkurugenzi wa taasisi hiyo Bi. Zena Mulokozi ameuambia mtandao huu kuwa, VLS tayari wameshawafikia wanawake zaidi ya 5000 Dar es Salaam na Pwani kuwapa elimu mbalimbali za ujasiriamali na kuwawezesha kwenda kupata mafunzo SIDO.
Amefafanua tasisi hiyo inawawezesha wanawake wapate mikopo kwa urahisi katika taasisi za kifedha ikiwemo na kuandaa matamasha mbalimbali ya kuwakutanisha wanawake pamoja na kuwajengea uwezo mbalimbali.
Amesema mwanamke yeyote ni mwekezaji na wanatakiwa wawe wathubutu katika kutenda na si kukubali kushindwa na kuacha utegemezi katika maisha yao ya kila siku kwani kufanya hivyo ndiko kunakowaletea ugumu na kujikuta wanajutia na kuwafanya wakutane na ukatili wa kijinsia.
Pia aliwataka kuwa waaminifu kwani uaminifu ndio silaha yao muhimu katika shughuli zao za kibiashara.
Ametaja changamoto kubwa inayowakabili wanawake wengi nchini ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiriamali hivyo kuwataka wawe na wasaa wajitokeze kupata elimu mbalimbali ikiwemo za ukatili wa kijinsia kutokana na wimbi kubwa lililopo sasa unyanyasi wa kijinsia.
Naye katika Mtendaji kutoka Baraza la kuwawezesha wanawake kiuchumi Taifa Beng’I Issa amewataka wanawake wajifunze kuweka akiba ili mitaji iweze kukua na kuweza kutimiza malengo.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na mikakati mingi ikiwemo kumuinua mwanamke kiuchumi na kumuwezesha kuachana na matumizi ya nishati chafu hadi ifikapo 2030.
Afisa Masoko UTT, Telesia Mrema aliwataka wanawake hao wawe na utamaduni wa kuwekeza fedha zao ili wapate faida kuliko kwenda kuweka fedha benki ambapo hakuna faida wanayopata.
Amefafanua UTT kuna uwekezaji wa kila aina ya uwezo wa mtu husika kuanzia elfu tano na kuendelea katika kifuko tofauti iliyoko na kujinyakulia faida ya asilimia kila mwezi katika mifuko hiyo




0 Maoni