Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Umoja Wanawake( UWT )Wilaya ya Ilala Fanta Boniface Kaijage, amegawa chakula na Futari kwa watoto wa makundi maalum wa kituo cha watoto yatima Msongola Wilayani Ilala.
Kaijage amegawa chakula hicho ikiwa ni wajibu wake kugusa makundi maalum yenye uhitaji ndani ya Wilaya ya Ilala kushiriki matukio ya kijamii.
"Nimegawa vyakula mbalimbali vikiwemo mchele ,Sukari, Maharage, sembe,Mafuta ,Sabuni,juice na mikeka ya kukalia katika kituo hichi cha watoto yatima Msongola pamoja na furari lengo na dhumuni kushirikiana chakula cha pamoja nao ili na wao wajione sawa na jamii nyingine "amesema Fanta.
Ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto wa makundi maalum ili na wao wajione sehemu ya jamii.
Mlezi wa Kituo cha Yatima Msongola Christina Haule, alisema kituo hicho kimeanzishwa mwaka 2004 kimesajiliwa mwaka 2006 kinapokea watoto wa aina zote kina watoto 89 na aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto wa makundi maalum.
Mmoja wa watoto wa makundi Maalum wa kituo hicho Stella Poul amesema alipokelewa katika kituo hicho akiwa Chekechea mpaka sasa anasoma shule ya Sekondari alitumia fursa hiyo kumshukuru Mjumbe huyo kwa kujitoa, kujali na kuwaletea misaada aliotoa katika kituo chao.


0 Maoni