Na Pilly Kigome-Nifahamishe News
DAR ES SALAAM
WAKALA wa Usajiliwa na Biashara na Leseni(BRELA) imewataka wafanyabiashara kuzingatia sheria ya usajili wa miliki bunifu kwa kutokupeleka alama zinazoenda kinyume na maadili ya Tanzania ikiwemo kutotumia rangi ya bendera ya Tanzania katika alama hizo.
Hayo yamesemwa na Afisa Usajili(BRELA) Ruth Mmbaga wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya kuelekea Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mmbaga amesema kuwa, katika maonyesho hayo wanaendelea kutoa elimu ya miliki bunifu ikiwemo alama ya biashara na huduma kwakuwa wamebaini changamoto ya wengi kukosa elimu hiyo.
Amesema watanzania wengi wamekosa utambuzi wa umuhimu wakusajili alama zao za biashara na kuendelea kutumia bila usajili hiyo wanakwenda kinyume na utaratibu na kujinyima haki zao zinazopatikana katika usajili huo.
Amefafanua faida ya kusajili alama ya biashara na huduma ni pamoja kuwasaidia wafanyabiashara tofauti wanaozalisha bidhaa aina moja kutofautisha bidhaa zao zinavyoingia sokoni.
Ingine ni kumuwezesha kwa urahisi kutangaza huduma yake sokoni, kuhimili ushindani katika soko kwani atakuwa na alama ya kipekee kutambulisha biashara yake.
Kumuwezesha mtumiaji wa bidhaa au huduma kuitambua kwa alama kutokana na kuwa na bidhaa nyingi za kughushi sokoni.
Mbali na hayo ingine inaweza Kumuingizia kipato kwa njia ya kuuza alama au kutoa haki ya matumzi kwa kukodisha mtu mwingine.
Mmoja wa wateja waliofika katika banda la Bw. Alexanda Mhagama amesema amefurahishwa na huduma zinazotolewa na BRELA kwa kuboresha huduma na hasa zinavyotolewa kidigitali.
“Nimefika hapa nimepata elimu nzuri ikiwemo na kuhudumiwa vizuri huduma niliyoihitaji yaani ingependeza na kutoa wito kwa Serikali taasisi zingine za umma waige mfano wa Brela” amesema Mhagama


0 Maoni