Na Pilly Kigome
KIBITI
TAASISI ya Kiislam ya Shia Ithinasheria (WIHPAS) imeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwawezesha kuwapa mitaji wanawake 320 Wilaya ya Kibiti Mkoa Pwani.
Zaidi ya Shilingi Mil.43 na laki2 zimetumika katika kutoa mikopo hiyo isiyo na riba katika vikundi 32 kwa wanawake kutoka Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA)Wilaya humo.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 10,2024 wakati wa ugawaji wa mitaji hiyo Mkurugenzi Mkuu WIHPAS, Shekhe Mohamed Hussein Rajeni(HAJISAHEB) amesema taasisi hiyo imeona iadhimishe maadhimisho hayo kwa kuwapatia mitaji wanawake wenye uhitaji ili waweze kuanzisha biashara ndogondogo watakazoweza kujikomboa kiuchumi, kusomesha watoto, kilimo, elimu na kujiendeleza katika dini.
Amesema mikopo hiyo iliyotolewa kwa wanawake hao haitakuwa na riba hata asilimia moja na hiyo itawafanya waachane na mikopo ya riba na ile mikopo umiza ambayo inawasumbua wanawake wengi katika jamii na hiyo ni kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluihu Hassan katika kuwakomboa wanawake.
Mbali na kutoa mikopo aliwaasa wanawake hao kutambua uwepo wa Mwenyezi Mungu kwa kujikita katika kupata elimu ya dini kwani itakuwa ni muongozo katika malezi ya watoto wao katika maisha yao ya kila siku kwani kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa watoto na vitendo viovu hasa uvunjifu wa maadili kila kukicha katika jamii ya Kitanzania.
Mwenyekiti JUMIKITA Wilaya Kibiti Salama Yahaya ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwaletea mikopo hiyo kwa awamu ya nne sasa na wamewezeshwa kujikwamua kwa kutoka hatua moja kwenda nyingine kwa kupitia mikopo hiyo.
Amefafanua wanawake hao wametokea katika kata sita ikiwemo Mjana, Matawanya, Kibiti,Dimani, Bungu na Mchukwi ambao wote wako katika muendelezo wa kupatiwa mikopo hiyo ambapo tayari imeshawasogeza wanawake katika biashara zao na wengine kuanzisha biashara.
WANAWAKE WA WILAYA YA KIBITI WAKIMSIKILIZA MKURUGENZIAidha waliiomba Serikali na taasisi hiyo wawawezeshe zaidi vifaa vya kilimo kama vile trekta, pembejeo, mbegu na dawa za kumwagilia magugu katika kilimo cha ufuta na mbaazi kwani wamekuwa hawana uwezo katika vitu hivyo.
Baadhi ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na taasisi hiyo ni Fatuma Mbonde ni mnufaika wa awamu ya tatu na aliweza kuanzisha biashara ya sabuni za miche na sasa tayari wameshafungua kiwanda kidogo kwa kuungana na wenzake wanne.
“Kwakweli tunaishukuru hii taasisi tumeweza kuanzisha kiwanda chetu wanawake watano tumeungana tunatengeneza sabuni za mche tunauza kujipatia faida na kuendesha familia zetu”amefafanua Mbonde




0 Maoni