Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
KAMATI ya Kupitia Kitita cha Mafao cha NHIF cha mwaka 2023, imewatoa hofu Watanzania kwamba hakuna atakayekosa matibabu kwa kuwa mkataba baina ya mfuko na watoa huduma za afya wa sekta binafsi (APHTA) haujavunjwa.
Akizungumza leo Februari 29,mwakahuu na vyombo vya habari,Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk Baghayo Saqware, amesema walitumia vigezo vyote kushughulikia malalamiko ya watoa huduma hao na hawajamwonea mtu yeyote.
“Kamati ilikuwa huru kumsikiliza kila mtu, tulikubaliana kwa pamoja na tuliamua kitita kianze kutumika kwa faida ya nchi na taasisi zetu.
“Kwa hiyo tunapenda kutoa msimamo wa kitaalam kwamba Wizara kupitia NHIF iendelee na utekelezaji wa kitita cha mafao kilichoboreshwa cha NHIF cha mwaka 2023 kama ilivyoshauriwa na kamati,” amesema Dk Saqware.
Kamati hiyo imesisitiza kuwa hakuna kituo kitakachositishiwa huduma na kama itatokea ameshauri watoe taarifa haraka katika mamlaka husika.
Maboresho ya kitita cha mafao cha mwaka 2023 yalianza tangu mwaka 2018 kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya iliyoelekeza mfuko kufanya mapitio ya kitita na bei zake kwa kuzingatia mwongozo wa matibabu nChini toleo la mwaka

0 Maoni