TUSIWE WAISLAMU MAJINA TUWASOMESHE WATOTO ELIMU YA DINI-UMMY

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKIZUNGUMZA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU


Na Pilly Kigome

DAR ES SALAAM

WAZAZI na walezi wametakiwa kujikita kuwarisisha watoto elimu ya dini kwani kufanya hivyo kutafanya watoto waweze kumtambua na kuwa na hofu ya Mungu na si kuwapa elimu dunia pekee.

Rai hiyo imeitowa leo Machi 17, 2024 jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa fainali ya mashindano ya kitaifa ya usomaji wa kuhifadhi kuruani tukufu.

Waziri Ummy amesema wazazi wanatakiwa  wawe na utamaduni huo kwani kutasaidia kujenga jamii bora katika maadili, na kujua na kupata utambuzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kinasema na kuamrisha nini ikiwemo kuwajenga kuwa na hofu na Mungu.

“Tusiwe waislamu majina ndugu zangu, tushikamane kwani kusoma dini kutaleta upendo, mshikamano, amani na utulivu” amefafanua

Hata hivyo amesema kuwapeleka watoto kusoma elimu ya dini ni lazima kwani ni amri ya MwenyeziMungu alisema IQRA” soma kwa jina la Mola wako” na kumaliza kwa kunukuu baadhi ya aya kutoka katika kitabu Tukufu Surat Bakara aya pili inayosema “ Hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake” amefafanua Mwalimu.

Mbali na hilo amewataka waumini wa dini hiyo wabadili mtindo wa maisha katika ulaji, kufanya mazoezi kwa wingi ikiwemo na kuwa utaratibu wa kufanya  uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kuepukana na maradhi yanayoshika kasi ya magonjwa yasiyoambukiza.



BAADHI YA WAUMINI WAKIFATILIA MASHINDANO HAYO

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Aisha Sururu (ASF) Amina Njechele amesema mashindano hayo Kitaifa ni ya 23 toka kuanzishwa kwa taasisi hiyo inayojishughulisha na mambo ya kidini na utoaji wa elimu kwa vijana.

Amesema awali wa kuanza mashindano hayo walikuwa na vijana wapatao 600 nchi nzima waliwachuja kwa viwango na walibaki 89 ndio walioingia fainali katika baadhi ya mikoa.

MWENYEKITI WA A.S.F BI AISHA SURURU AKIZUNHUMZA NA WANAHABARI

Hata hivyo amesema ASF wanakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo na kuanza ujenzi katika eneo lao kubwa lililopo Kiparanganda mkoani Pwani.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza kwa upande wa kuhifadhi juzuu 10 upande wa wasichana alikuwa ni Ashura Bugoma mkazi wa Dar es salaam aliyepata alama 98.66 alijinyakulia kitita cha Sh. Mil.3.

Kwa upande wa juzuu 20 mshindi kwa upande wa wasichana alikuwa ni Halima Hamisi Mbaraka mkazi wa Dar es Salaam amepata alama 99 alijinyakulia kitita cha Sh.Mil.4

Kwa upande wa wavulana alikuwa ni Juma Ali Abdallah mkazi wa Dar es Salaam amepata alama 98.75 nae alipata kitita hicho.

Washindi wa jumla katika mashindano hayo wa juzuu 30  kwa upande wa wasichana alikuwa ni Saima Hassan Selemani alipata alama 99.25 na mvulana alikuwa ni Amir Maulidi Dundo aliyepata alama 99.

Wote kwa pamoja walijinyakulia zawadi ya nyumba na kitita cha Sh.Mil.5 kila mmoja kutoka kwa Rais Samia Sululu Hassan Sh.Mil.3 kutoka ASF na Mil 2 kutoka kwa Waziri Ummy


Chapisha Maoni

0 Maoni