Na Mwandíshi Wetu
DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh 38,409,560 kutoka kwa wadau wa maendeleo shirika la JHPIEGO ambao wanashirikiana na Mkoa katika Kuboresha huduma za afya ya uzazi, mtoto na vijana Balehe ( Reproductive Maternal Neonatal Child and Adolescent Health)
Tukio hilo limefanyika leo March 25 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amewashukuru shirika la JHPIEGO kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya ambapo ndani ya Kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Mkoa umeshudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya Afya ya msingi wa takribani Bilioni 52 katika miradi zaidi ya 70 ya ujenzi wa miundombinu na Bilioni sita katika ununuzi wa vifaa na vifaa tiba mbalimbali.
Aidha RC Chalamila amewataka wataalam kuvitumia na kuvitunza vizuri na kuvifanyia matengezo ya vifaa hivyi ili viweze kudumu muda mrefu.
Hata hivyo RC Chalamila mara baada ya kupokea vifaa tiba hivyo amevikabidhi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa ili viweze kwenda kutumika kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii.



0 Maoni