Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
MANISPAA ya Kinondoni bado inaendelea kuwa kinara kwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa Matende na Mabusha kwa kiwango cha asilimia 2.3.
Kata kumi kutoka Manispaa hiyo ambazo ni Tandale, Kijitonyama, Mwananyamala, Kigogo, Mzimuni, Ndugumbi, Hananasif, Kinondoni na Makumbusho ndizo zinaendelea kutengeneza maambukizi mapya ya magonjwa hayo.
Hayo yamesema leò jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kutoa tathimini ya magonjwa hayo.
Waziri Ummy amesema kuwa, maambukizi makubwa ya ugonjwa huu yalikuwa katika Halmashauri 119 nchini ambapo watu Million 31.2 walikuwa katika hatari ya kupata mambukizi ya vimelea vya ugonjwa huu.
Amesema hadi kufikia sasa Serikali kwa kushirikiana na wadau wameweza kudhibiti ugonjwa huo katika Halmashauri 112 kati ya 119 na kubakiwa na Halmashauri 7 ambazo ni Kinondoni, Pangani, Mafia, Kilwa, Lindi Manispaa, Mtama na Mtwara Mikindani.
Amefafanua kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam mwezi Machi na Agosti 2023 na Februari 2024 Wizara ya Afya kushirikiana na uongozi wa Mkoa Dar es Salaam walifanya tathimini ya kiwango cha maambukizi ya magonjwa hayo na kupata matokeo tofauti ikiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Ubungo walibaini hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa wa mabusha na matende kwa kipindi cha miezi sita baada ya kusitisha umezeshaji wa Kingatiba katika Hamashauri hizo
“Hivyo kwa matokeo haya Wizara ya Afya tunasitisha kampeni za umezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa wa matende na mabusha katika maeneo husika ambayo hayana maambukizi mapya ambayo ni Manispaa ya Temeke na Kata 10 Manispaa Kinondoni.
Mratibu Udhibiti wa Ugonjwa wa Mabusha na Matende Wizara ya Afya Dr. Faraja Lyamuya alisema Serikali iko katika jitihada za kutokomeza magonjwa haya ambapo kupitia mkutano wa “Reaching the last Mile” uliofanyika mwezi Disemba mwaka 2023 huko Dubai Rais Samia Suluhu Hassan aliweka kiasi cha Dola za Kimarekani Milion tatu katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka huu 2024.
Dr. Lyamuya amesema katika baadhi ya maeneo ambayo maambukizi haya yanapatikana kwa sana na kutoisha kwa ugonjwa huu ni kutokana na kuhamahama kwa wakazi kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hali ya hewa ya kimazingira.
“Tunawaasa wananchi wajitokeze pinddi wanaposikia mkampeni za kutokomeza magonjwa hayo yanaendelawkani wataweza kupata afursa za matibabu na dawa kwani dawa hazipatikani katika maduka ya dawa ya kawaida” alifafanua.

0 Maoni