Na Moshi Saidi
DAR ES SALAAM
MUFTI MKUU Dr. Abubakar Zubeir Ali Mbwana amewataka waislamu wa Tanzania kutazama Mwezi kwa Makini siku ya Jumatatu tarehe 11.3.2024 sawa na Shaabani 29.
"Leo ni Mwezi Shaabani 25. Jumatatu ijayo ni shaabani 29. Mkiona Mwezi siku hiyo ya Jumatatu popote mlipo kote nchini toeni taarifa haraka iwezekanavyo kwenye ofisi ya Bakwata ya karibu ili funga ya Ramadhani ianze Jumanne 12.3.2024. ikiwa hautaandama Jumatatu tutatimiza siku 30 za shaabani na kuanza funga Jumatano 13.3.2924" amesema Mufti
Akiongea na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake jijini Dar es salaam Mufti amewataka Masheikh kuendeleza utaratibu wa kutoa Darsa misikitini na kuwataka waislamu kusikiliza dasra hizo.
Aidha amewataka waislamu wazidishe dua na ibada mbalimbali ambazo zina malipo makubwa ndani ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
.......

0 Maoni