Na Pilly Kigome
MONDULI-ARUSHA
JAMII ya WAMAASAI wamemtunuku jina la kimila Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuvutiwa na uongozi wake ikiwemo kuiendesha vizuri nchi ya Tanzania.
Hayo yamesemwa leo Februari 16 na Kiongozi Mkuu wa Kimila wa Jamii ya Wamaasai Tanzania, Isack Olekisongo Meijo nyumbani kwa Marehemu Lowasa katika kijiji cha Ngalash Monduli Mkoani Arusha alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari.
Kiongozi huyo wa kimila amesema wamempa jina maalum la kimila Rais Samia Suluhu Hassan lililotambulika kwa jina la ‘NIOMOOM’ ambalo lenye maana kiongozi wa Baraka katika utawala wake.
Amefafanua wametoa jina hilo kwa Rais huyo kwakuwa ni kiongozi aliyeiheshimisha jamii ya kimasai hasa katika mchango wake mkubwa katika mazishi ya marehemu Lowasa na anayejitoa katika Taifa lake kusaidia watu katika kila nyanja kukuza uchumi.
“Rais Samia anaiheshimisha nchi, hali ya uchumi nchini inazidi kuimarika ikiwemo na kudumisha amani nchini jambo kubwa sana na tumeona tumzawadie jina hilo kutokana na sifa hizo zote” amefafanua
Akieleza wàsifu wa marehemu amesema Lowasa ndio aliyewahamasisha katika swala zima la elimu na kutokomoeza mdudu ujinga katika jamii hiyo ikiwemo na kuwaelimisha kuacha baadhi ya mila potofu ikiwemo ukeketaji sema wamepata pigo kubwa sana ambalo , kutoa meno, kutoboa masikio, kungo’oa meno.
Amefafanua kitu kikubwa ambacho hawataweza kumsahau ikiwemo na harakati zake za kupinga umasikini katikajamii hiyo amekuwa akielimisha jamii hiyo kuondokana na ufukara katika jamii hiyo kwa kutoa elimu za mara kwa mara ikiwemo kuwapeleka nchi wamasai nchi jirani ikiwemo Uganda na Kenya kuwafundisha jinsi ya ufugajibora unavyotakiwa kuwa na ufugaji wenye tija.
“Alishawahi kufanya makongamano makubwa kutukutanisha sisi viongozi wajamii hii wamaasai wa Tanzania na Kenya kutuweka pamoja ili tuweze kutambuana na kujadli mambo ya jamii hiyo” amesema
"Vilevile tumeweza kuachana na baadhi ya tamaduni za zamani ambazo hazina tija katika jamii yetu ikiwemo ukeketaji, kun'goa meno, kutoboa masikio kwakuwa tumeshajua madhara yake na hii yote ni juhudi za marehemu Lowasa" amesema
.jpg)
0 Maoni