WAKAZI KARIAKOO WALALAMIKÌA KELELE ZA MSIKITI USIO RASMII

 

JENGO LILILOPO MTAA WA LIKOMA NA NARUNG'OMBE LINALODAIWA KUSABABISHA KELELE 

Na Mwandishi  Wetu

DAR ES SALAAM

BAADHI ya Wakazi wa Kariakoo Mtaa wa Likoma na Narung’ombe wanamlalamikia mkazi mwenzao kwa kusababisha kelele kwa kugeuza nyumba ya makazi kuwa msikiti na na kusababisha kelele nyingi hatarishi kwa wakazi hao.

Imedaiwa kuwa mkazi huyo anayemiliki moja ya jengo katika mtaa huo ameanzisha msikiti hewa juu ya jengo hilo na kufunga vipaza sauti(spika) kubwa zaidi ya tatu na kusababisha kelele usiku kucha hali inayoleta taharuki kwa wakazi hao.

Wakizungumza na Mtandao huu baadhi ya wahanga wanaoathirika na kelele hizo waliioombaa majina yao yahifadhiwe wamesema kuwa, mmiliki wa jengo hilo la ghorofa nyumba No.69 iliyopo Mtaa wa Likoma na Narung’ombe mwenye asili ya kiarabu amegeuza nyumba hiyo ya makazi kuwa msikiti na kusababisha kero na adha kutokana na kelele nyingi kutoka kwenye vipaza sauti.

Wamesema kutokana na kelele hizo zinazopigwa usiku kucha kutoka katika nyumba hiyo zinawashangaza kwa kuwa zinaenda kinyume na taratibu ukilinganisha  na misikiti mingine ambayo ipo katika eneo hilo.

“Sisi tunachoshangaa mbona kuna misikiti ipo karibu ambayo tunajua inafanya kazi za Mungu haipigi kelele kama hilo jengo, kuna misikiti mingi pale karibu  ukiwemo Msikiti wa Idrisa na mingine, Sisi hatujawahi kuona inapiga kelele usiku kucha”wamesema

Aidha wamefafanua tayari wameshawasilisha barua ya malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila na NEMC kwa kuwa walisharipoti kituo cha Polisi lakini hawajapata msaada hadi sasa.

“Tunaomba mamlaka husika watusaidie katika jambo hili tunateseka kwa makelele kwani kuna wagonjwa, wajawazito, watoto, kelele hizo zinatufanya wengine tukalale nyumba za wageni mbali na hapo kukwepa kelele hizo” amesema

Hata hivyo Afisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ndugu Emile amesema  malalamiko hayo tayari  yameshafika kwao na tayari wameshaanza kuyafanyia kazi.


“Tayari tumeshaanza kushughulikia malalamiko hayo ya wakazi hao kuhusiana na kelele hizo tunalifanyia kazi naamini mambo yatakuwa sawa tutapokutanisha pande zote mbili” amefafanua

Chapisha Maoni

0 Maoni