MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALBERT CHALAMILA
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amekutana na kufanya kikao na Viongozi waandamizi wa DAWASA na TANESCO Ofisini kwake Ilala Boma.
Akizungumza wakati wa kikao hicho leo Februari 26 RC Chalamila amezitaka Taasisi hizo kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja na kuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi ili kuwa na uzalishaji wenye tija utakaopelekea kutoa huduma bora kwa Jamii wakati wote
Aidha RC Chalamila amesema Dar es Salaam ni hub ya kibiashara, hub ya kidiplomasia, hub ya kiuchumi na vingine vingi,vinavyofanana na hivyo, umeme au maji vikikosekana kuna hatarii kubwa ya kudhorota kwa mnyororo mzima wa uchumi wa nchi.
" Natamani kuona Mkoa wa Dar es Salaam hauna changamoto au migao ya aina yoyote ya umeme wala maji kutokana na umuhimu wa Mkoa huu katika makuzi ya uchumi wa nchi" Amesema RC Chalamila
VIONGOZI DAWASA TANESCO WAKIWA KATIKA KIKAO KAZI MKAKATI NA MKUU WA MKOA LEÒSambamba na hilo amesema umeme ukiwepo maji huzalishwa kwa wingi na maji yakizalishwa kwa wingi husaidia kwa sehemu kubwa kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
Akiwa katika ziara zake za kutembelea miradi ya maendeleo ya utekelezaji jijini Dar es Salaam na baadae kuongea na wananchi katika mikutano ya hadrara kupokea kerò za wakazi wa Dar es Salaam malalamiko mengi yalikuwa ni umeme na maji.
Katika mikutano hiyo ambayo tayari ameshafanya Temeke Lumo na Mwananyamala na Kimara wakazi wengi wa jiji wamekuwa wakimlalamikia RC kukosa huduma hizo muhimu kwa vipindi virefu.
Leo Februari 26 RC Chalamila anaendelea na ziara yake katika Jimbo la Ubungo.



0 Maoni