RC CHALAMILA AWAPA DAWASA SIKU 7 KURUDISHA MAJI

MKUU WA WILÀYA 
YA KINONDONI AKIMUELEKEZA JAMBO MKUU WA MKOA WA ĎAR E SALAAM KUHUSIANA NA MIRADI YA UTEKELEZAJI YA JIMBO LA KINONDONI


Na Pilly Kigome

DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam amewapa siku saba Mamlaka ya Maji Safi (DAWASA) kurudisha maji katika baadhi ya maeneo yaliyokosa maji kwamuda mrefu katika Jimbo la Kinondoni.

Agizo hilo amelitoa Februari 21 mwaka huu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara na kupokea kero za wananchi wa Jimbo la Kinondoni katika viwanja vya Mwananyamala Mwinjuma Kata ya Makumbusho, Mtaa wa Kichangani.

Chalamila ameitaka DAWASA warudishe maji  kutokana na kilio kikubwa cha wananchi cha ukosefu wa maji wa zaidi ya wiki moja katika baadhi ya maeneo.

Akijibu malalamiko hayo, Kaimu Meneja wa DAWASA Kinondoni Frank Sulley amesema kuwa, ukosefu huo wa maji jimboni humo unasababishwa na ukosefu wa umeme na kuharibika kwa miundombinu ya mifumo ya maji uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha nchini.

Alimefafanua maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kijitonyama, Ali Maua A na B, MasakiMwisho na MWananyamala Kisiwani.

Imedaiwa hadi kufikia jana maeneo hayo ni zaidi ya wiki moja maji hayajatoka mabombani.

Awali Mkuu wa Mkoa huyo alianza kwa kukagua miradi  mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambapo alizindua mradi Shule ya Mchepuo wa Kiingereza iitwayo Richard Mgana iliyopo Kata ya Kigogo.

Jengo hilo linatarajiwa kuwa na vyumba 18 vya madarasa, matundu 30 ya vyoo, jingo la utawala na kichomeo taka.

Akizungumza eneo la tukio Mbunge wa Kinondoni Abbas Tarimba amesema katika kata 20 za Kigogo wameweka matarajio katika kila kata kuwe na shule ya mchepuo wa kiingereza.

JENGO LA GHOROFA MOJA KITUO CHA AFYA KINONDONI 

Vilevile Mkuu huyo alizindua jengo la ghorofa moja lenye wodi ya wazazi, sehemu ya upasuaji na wodi ya wagonjwa  ndani (IPD) kituo cha afya Kinondoni.



Chapisha Maoni

0 Maoni