Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
MBUNGE wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Ladislaus Kamoli anatarajia kuendelea na zoezi la kufanya ziara ya kukagua miundombinu katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo.
Lengo la ziara hizi nikuona miradi ya maendeleo ya miundombinu inayofanyika ikiwemo na kusikiliza changamoto za wananchi ili akazitafutie ufumbuzi.
Ziara hiyo itajumuisha Kata za Kinyerezi, Vingunguti na Mnyamani zote za jimboni humo.
Ziara hiyo inatarajiwa kufanyika February 28, mwakahuu.
Mhe.Bonnah amekuwa ni Mbunge anayesimamia kwa nguvu zote maendeleo ya jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa barabara ikiwemo na Shule za Msingi na Sekondari.

0 Maoni