Na Pilly Kigome
MONDULI ARUSHA
KIFO cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowasa kimewapa funzo kubwa MACHIFU kwa kuwaachia alama na mafunzo mengi ikiwemo upendo na kushikamana.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Machifu Tanzania Antonia Tonesiza Sangalali leo Februari 17 katika kijiji cha Ngalash Monduli Mkoani Arusha mara baada ya kukamilika kwa mazishi yake katika kijiji hicho.
Sangalali amesema kupitia maisha aliyokuwa akiishi Lowasa wamejifunza mengi makubwa kama machifu wa nchi hii kubwa ikiwa ni tuwe na upendo na kutokubagua watu katika jamii zetu zilizotuzunguka.
“Kwa kweli marehemu Lowasa ametufundisha upendo, kushikamana, kushirikiana ikiwemo hata kula pamoja nakutobagua watu katika maisha yetu ya kilasiku”
“Mfano mkubwa ni ule alikuwa akichinja ng’ombe zaidi ya 12 katika kila sikukuu anajumuika na wananchi kwa kula pamoja” amefafanua
Aidha amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo kwani umegusa watu wengi wa kila hali wa kati, wa juu na wa chini kwani marehemu alikuwa hana ubaguzi wa dini,ukabila wala rangi alikumbatia watu wote.
Hivyo kupitia maisha aliyokuwa akiyaishi Lowasa kwao ni funzo kubwa sana sana kutokana na matendo yake mema aliyokuwa akiyafanya katikamaisha yake.

0 Maoni