Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amewataka wapinzani hasa CHADEMA kusema ukweli kuhusiana na maridhiano yaliyopatikana ikiwemo na kuweka wazi kuwa Serikali iliwapa Shilingi Bil.2.7 za ruzuku za miaka mitatu.
Pia amewataka kutambua nia njema iliyooneshwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutaka maridhiano inapaswa kuendelezwa na kuenziwa kwa vyama vyote vya siasa.
Aidha, amevishauri vyama vya siasa vya upinzani hususani CHADEMA kuacha kufanya maandamano yasiyo na msingi badala yake wathamini utayari wa Rais Samia katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa katika maendeleo yakiwemo ya demokrasia.
Kinana ametoboa tobo katika mkutano wake wakati akizungumza na wanachama wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Februari 4 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond.
Amesema maridhiano yaliyoingiwa kati ya CCM, CHADEMA na vyama vingine vya upinzani nchini yameleta tija na yataleta tija kwani vyama hivyo vinaweza kuongea lugha moja katika meza moja ukitofautisha na siku za nyuma.
Amefafanua kupitia maridhino hayo CHADEMA wamenufaika kwa kiwango kikubwa kwani kulikuja na hoja 11 na zote ni za kwao na kati ya hizo CCM hawakuwa na hata moja na zote zimeweza kufanyiwa kazi ikiwemo na hiyo ruzuku waliyopewa ambayo waliisusia kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Amefafanua faida nyingine iliyopatikana kuatokana na maridhiano hayo ni ile wafuasi wapatao 400 wa chama hicho waliokuwa mahabusu kwa sababu toauti karibia wote waliachiwa huru isipokuwa kesi mbili ambazo hizo zina mlolongo mrefu wa kisheria ikiwemo ile iloiyopo mkoani Njombe inayohusu tuhuma za mauaji na ile ya Kibaha inayohusu tuhuma za dawa za kulevya.
Akielezea kuhusu sheria mpya, amesema pamoja na uzuri wake ikiwemo kuzingatia maoni ya wadau wakiwemo CHADEMA wenyewe, lakini bado kinasema haifai.
"Nilifikiri sheria hii mpya wangesema itatufikisha mbali zaidi, lakini wao wanasema hii haifai, basi turudi kule. Sheria ya sasa ni bora kwa muundo, kwa maudhui, kwa malengo, kwa dhamira sijui mnanielewa?. Nitumie nafasi hii kuwasihi ndugu zangu wa CHADEMA waungane na Watanzania waachane na mandamano, waangalie dhamira ya Rais.
“Hivi Rais na baraza lake la mawaziri kama wasingepeleka hii sheria mpya ya uchaguzi nani angemlazimisha? Lakini Rais busara imemuongoza akasema hapana hebu twende pamoja na mimi ndio mtetezi mkubwa wa maridhiano na ustahimilivu.
Aidha ametumia nafasi hiyo kufafanua kwa kina ubora wa sheria yaauchaguzi ambayo imepitishwa na bunge hivi karibuni baada ya wadau mbalimbali nchini kutoa maoni ambapo amesisitiza sheria hiyo ni bora kuliko iliyopo sasa.




0 Maoni