HOTEL LIVERPOOL YATANGAZA KUTOA HUDUMA SAA24, YATOA AJIRA KWA VIJANA

MENEJA WA HOTEL YA LIVERPOOL SALIM ABDALLAH AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI


KOROGWE-TANGA

HOTEL ya LIVERPOOL iliyopo Korogwe mkoani Tanga imetoa ajira zaidi ya 30 kwa vijana katika kada tofauti ikiwa ni kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika utoaji ajira wa kundi hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Februari 18, Meneja wa hotel hiyo Bw. Salim Hussen Abdallah amesema wamejipanga vyema kuhudumia wasafiri wamikoa ya Kaskazini kutokana na huduma za viwango vya juu zilizopo hapo.

Amesema wamefanya uwekezaji mkubwa wenye thamani ya zaidi ya Milioni 500 ili kuhakikisha kila mmoja anafikiwa kwani kuna huduma tofauti kwa makundi maalumu kila mtu kulingana na uwezo wake.

Amebainisha watanzania na wasiwe na wasiwasi kuhusiana na huduma kwani wamejipanga vilivyo kutoa huduma kwa masaa 24 kwani wanatambua kuna wasafiri wanasafiri usiku baada ya serikali kuruhusu hilo.

“Usalama katika hoteli yetu ni wa kutosha, tunawahakikishia Watanzania waje kwa wingi katika hoteli yetu hii pendwa na kubwa tunatoa huduma hata za VIP na VVIP” amefafanua Abdallah.

“Tuna dhamana ya kuwahudumia wananchi kwa mujibu wa sheria hivyo wasafiri wajitokeze kwa wingi kufika hotelini hapa na vyakula ni bei ya kawaida kabisa” amefafanua

Chapisha Maoni

0 Maoni