Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imewataka wananchi kukimbilia maonesho ya sheria yanayoendelea ili kuweza kupata elimu kuhusiana na masuala ya haki za bima.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Sheria Ponziano Lukosi akizungumza katika manesho hayo Januari 29 jijini Dar es Salaam.
Amewataka wananchi kuyatumia vyema maonesho hayo kwakuwa hiki ndio kipindi cha wananchi kuweza kutambua vyema sheria na haki zipatikanazo kuhusiana na masuala mazima ya bima za aina zote nchini.
Amefafanua uhusiano wa Tira na maonesho hayo ya wiki ya sheria ni kwamba wana uhusiano wa moja kwa moja kwa kuwa wao ni chombo cha kusimami sheria endapo kunajitokeza migogoro ya kibima kati ya mteja na mtoa huduma ya bima.
Amefafanua kunapotokea migogoro ya kibima na shauri hilo kufikishwa mahakamani TIRA inachukua muongozo wa hukumu aliyeshinda basi ndie atakayepata stahiki kwa kupitia hukumu hiyo.
Afisa Uhusiano kwa Umma,Tabia Mchakama ameiambia Nipashe kuwa,TIRA ina mamlaka ya moja kwa moja ya kusimamia migogoro ya kibima kusimamia haki kutokana na Sheria No.10 Sura ya 394 ya mwaka 2009 sheria ya bima ndio inawapa muongozo ni jinsi ya upatikanaji wa haki ya migogoro hiyo.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kujitokeza wanaposikia maonesho hayo ya sheria kwani kwa kupitia Tira wataweza kupata utambuzi wa jinsi gani wataweza kupata haki zao endapo watakutana na migogoro ya kupata stahiki zao kwa ajili ya Ustawi wa Taifa” amesema.
Kauli mbiu ya mwakahuu kupitia maonesho hayo ya Sheria yaliyoandaliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam TIRA- Kwa Soko Salama la Bima.


0 Maoni