Na Pilly Kigome
DAR ES SALAAM
NAIBU Waziri Muungano na Mazingira (MNEC) Khamis Hamza Chilo amewataka wanachama wa Jumuiya ya wazazi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto katika jamii ili kuwe na kizazi bora katika Taifa la Tanzania.
Mbali na malezi Chilo aliitaka jumuiya hiyo kusimamia maadili na elimu kwani hiyo ni kazi na majukumu kubwa ya jumuiya hiyo.
NAIBU WAZIRI MUUNGANO NA MAZINGIRA, KHAMIS CHILO AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO MKUU ILALAChilo alitoa maagizo hayo katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala ulioandaliwa na kamati ya utekelezaji wa kata hiyo.
Ameitaka Jumuiya hiyo kwenda kusimamia sekta ya elimu kwa kushirikiana na walimu ili kuweza kupata viongozi bora wa taifa la kesho ambalo litaweza kuibua na kuleta viongozi bora ambao watakuja kusaidia Chama cha Mapinduzi.
Amesema sasa hivi jamii inakabiliwa na changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili ikiwemo vitendo vya ukatili katika jamii hivyo kuitaka juiya hiyo kuweka kipaumbele majambo hayo na si kuangalia madaraka na mambo yao binafsi na kuacha kuiangalia jamii.
Aidha amewataka na kuwaasa wana chama wa CCM kuondoa makundi na kuwataka wawe kitu kimoja na kutokuwa na uroho wa madaraka kwani uongozi mtu anapangiwa na Mungu hivyo wawe wamoja ili kuhakikisha CCM inashika dola 2025 kwa kuwasimamisha wabunge na Rais kutoka chama hicho.
“Hayo yote tutayapata kama tutakuwa kitu kimoja, hivyo tushikamane, tusimame pamoja kwani tunajenga nyumba moja “ amesisitiza
Wakati huohuo aliitaka jumuiya hiyo suala zima la kusimamia mazingira kwani kuna watu bado wanaojihusisha na uharibifu wa mazingira kwa kuendelea kuzalisha mifuko ya plastiki ambayo tayari imeshapigwa marufuku.
“Watu wote wanaoharibu mazingira serikali itawachukulia hatua bila kuwaacha wale wanaoharibu vyanzo vya maji watachukuliwa hatua kali na wananchi mtoe tarifa pindi mnapowaona” ameonya Chilo.
MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI KATA YA ILALA SABRY SHARIF AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA HIYO
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala, Sabry Sharif amesema kata hiyo iko imara katika utendaji wake kukipigania Chama cha Mapinduzi kwani inashirikiana vyema na Jumuiya zote za chama hicho ikiwemo na ushirikiano wa kata zingine na ngazi ya Wilaya na Taifa.
Sharif amesema kata hiyo imejikita vyema katika kukitetea chama cha Mapinduzi na kuunga mkono juhudi azifanyazo Rais Samia Suluhu Hassan katika kulijenga Taifa kwa kuwa bega kwa bega katika juhudi hizo katika nyanza zote .
Kata hiyo imeweza kugawa kadi kwa wanachama wapya zaidi ya 50 na kupawa kiapo cha utiii kutoka Chama cha Mapinduzi.




0 Maoni