Mwenyekiti Wazazi Kata Ilala Sabry Shariff, kulia aliyesimama akiwa katika moja ya kaya ya wahanha w mafuriko
DAR ES SALAAM
Na Pilly Kigome
KATIKA kuonyesha uzalendo na uongozi uliotukuka ni lazima uwe kipaumbele katika mambo ya kijamaa ikiwemo majanga, maafa yanayowakuta wananchi waliokuzunguka ama walio mbali yako ili hali umeguswa na majanga hayo.
Mwenyekiti Jumuiya ya Wazazi (CCM) Kata ya Ilala CDE.Sabry Shariff ametoa mkono wa pole kwa wahanga zaidi ya 250 waliokumbwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea nchini.
Shariff ametoa mkono huo katika eneo la Mivinjeni jijini Dar es Salaam kwa kuwawafariji ikiwemo pamoja na kula nao chakula cha pamoja na wahanga hao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii amesema akiwa kama kiongozi wa Jumuiya ya Wazazi ameguswa na akiwa kama kiongozi ni wajibu wake kuiangalia jamii inayowazunguka.
“Kiukweli nimeguswa hadi kupelekea kufanya hivi, nashukuru nimekuja kuwaona wahanga kuwapa chochote nilichojaaliwa na Mwenyezi Mungu hii ikiwa ni kuwafariji wenzetu” amesema Sabri
Mwenyekiti Sabry katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa UVCCM wa Kata hiyo.Amesema katika mafuriko hayo eneo hilo hakuna mtu aliyepoteza maisha bali ni upotevu wa mali kwa baadhi ya familia uliotokana na mvua hiyo kubwa.
Mhanga aliyejitambulisha kwajina moja la Mama Chezo amesema wamepokea kwa furaha ugeni huo kwani uliwafariji kwa kiasi kikubwa kwa kuona Chama Cha Mapinduzi kinajali na kuthamini watu wao
“Kwakweli tunaomba Viongozi wengine wa Chama hiki kiwe mfano wakuiga kuwafariji wananchi wao waliowazunguka na si kuwathamini kipindi cha kampeni pekee, hii inapelekea hadi watu baadhi kuchukia siasa” amesema Mama Chezo.
.jpg)
.jpg)
0 Maoni