DAR-ES-SALAAM
Na Pilly Kigome
KUTOKANA na changamoto za ukosefu wa maji nchini Chuo cha Maji kinajipanga kuanzisha vyanzo vipya vya maji ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Kuwaboreshea mafunzo ya kitaaluma ya miundombinu nje ya nchi walimu 20 wabobezi 12 katika ngazi za shahada ya uzamivu(PhD), watano Shahada ya Umahiri (Masters) na watatu katika ngazi ya Shahada ya Uangavu(Bachelor Degree).
Akizungumza katika mahafali ya 47 ya Chuo cha Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu amekitaka Chuo hicho udahili wa wanafunzi uendane na kasi na ubora wa mahitaji yaliyopo.
Katundu amekitaka chuo hicho kiandae mitaala ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ikiwemo masomo ya ujasiriamali ndani ya chuo hicho ili kuwajenga umahili na kujitegemea katika sekta ya ujasiriamali pindi wamalizapo masomo.
Ikiwemo wawe na ubora na tija wenye uwezo mzuri wa kutatua changamoto za maji zilizopo nchini.

Mbali na hilo amesema wamenunua hekari tano katika kampasi ya Singida ili kupanua miundombinu mbalimbali katika sekta hiyo.
Jumla ya 682 wamehitimu katika mahafali hayo ya 47 ambapo wameshadahili wanafunzi 2197 mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 59 ukilinganisha na mwaka 2022 walidahili wanafunzi 1384.
Hata hivyo amesema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya watumishi ikiwemo miundombinu kwa kukosa maeneo ya kufanyia mihadhara.
0 Maoni