ZANZIBAR
CHAMA cha Waandishi wa
Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,
ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake
Zanzibar (ZAZELA) na Jumuiya ya
Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba
(PEGAO) kupitia mradi wa kuinua
Wanawake na Uongozi, wameandaa tunzo
maalum ya uandishi wa habari za
Takwimu za wanawake na uongozi ikiwa ni
katika maadhimisho ya
kuelekea siku ya wanawake duniani
Kufuatia taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema kuwa tunzo hizo ni muendelezo wa
shughuli zinazofanywa na mradi wa
kuinua wanawake na uongozi kufikia
50/50 katika ngazi zote.
Taarifa hiyo imesema
kupitia
tasnia ya habari itawashajiisha
waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbal ikiwa na lengo la kutumia
vyombo hivyo vya habari ili
kushajiisha masula ya wanawake na
uongozi.
Tunzo hii itahusisha
kazi zilizotolewa katika vyombo vya habari vya aina
nne (4) ambavyo ni
Uandishi wa habari za Makala katika
magazeti (feature articles)
Uandishi wa habari wa vipindi katika
redio (radio program)
Uandishi wa habari katika Televisheni
(TV program) na
Uandishi wa habari wa makala katika
mitandao ya kijamii (feature articles in
social media story).
Hivyo, TAMWA ZNZ na
washirika wake inawaalika waandishi wa habari
kukusanya kazi zao au kuandika katika
eneo hilo na kuziwasilisha kwa wakati.
Imesema Kipindi cha
Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe
katika ubora unaostahiki wakati
Kipindi au makala iliyochapishwa au
kurushwa hewani katika vyombo
mbali mbali vya habari vikiwemo
magazeti, runinga, redio na mitandao ya
kijamii katika kipindi cha kuanzia
Januari 1 hadi Disemba 31, 2023.
Sambamba na hayo TAMWA
ZNZ kwa kushirikiana na wadau wake wametoa wito kwa wanahabari kujiendeleza
zaidi katika fani lakini pia taasisi za habari pamoja na vyombo vya habari
kuimarisha mafunzo ya muda
mfupi na muda mrefu kwa waandishi wa
habari.
“Waandishi wa habari
tufahamu kuwa kazi hii ni kusaidia jamii na hivyo ni
muhimu kutumia kalamu na vipaaza sauti
katika kuelimisha na kuibua kero
na sauti za wasio na sauti”imesema
sehemu ya taarifa hiyo
Amesema ni muhimu kwa
waandishi na wahariri kuimarisha kada hii kwa kufuata kwa
vitendo maadili ya habari lakini wito
kwa wahariri kuwasaidia waandishi
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hii ni mara ya tatu
kufanyika tunzo ya aina hii ambapo mwaka jana 2022
jumla ya waandishi kumi walishinda
tunzo za umahiri kwa upande wa
magazeti na mitandao ya jamii.
Kazi ziwasilishwe katika ofisi ya Chama
cha ya Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA,
ZNZ) Tunguu karibu na IPA na
Kwa Pemba kazi ziwasilishwe katika
ofisi ya Tamwa Chake chake Pemba.
0 Maoni